Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WADAU 600 na mifuko zaidi ya 60 ya uwezeshaji kutoka sekta za umma na binafsi wanatarajiwa kushiriki kwenye kongamano la saba la uwezeshaji wananchi kiuchumi litafanyika Jijini Dodoma tarehe 29 mwezi huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa pamoja na Shirika la Care Tanzania na Mfuko wa Fedha wa Self chini ya Wizara ya Fedha, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema kongamano la mwaka huu litakuwa la kipekee ukilinganisha na yale yaliyopita.

“Viongozi serikalini wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na makatibu tawala wote, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa maendeleo wa wilaya zote zilipo katika mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani, wakuu wa taasisi za serikali na viongozi kutoka sekta binafsi watashiriki kwenye kongomano,” alisema Bi. Issa.

Bi. Issa alisema waratibu wote wa uwezeshaji kutoka mikoa yote nchi nzima watakuwepo kwenye kongamano ambalo litaongozwa na Waziri Mkuu, Bw. Kassim Majaliwa ambapo ripoti maalum kuhusu uwezeshaji litazinduliwa wakati wa kongamano.

“Kongamano la hili ni muhimu sana katika sekta au tasnia ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwani ni kipaumbele kikubwa cha serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan,” alisema Bi. Issa na kuongeza kuwa kongomano litatanguliwa na maonesho ya wiki ya uwekezaji yatakayoanza septemba 26 hadi 28.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa Mfuko wa Fedha wa Self kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Petro Mattaba alisema mfuko wake unafanya kazi karibu sana na Baraza la Uwezeshaji na mpaka sawa watanzania 240,000 wameshanufaika mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 228.

“Tuna matawi kwenye mikoa 12 ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Shinyanga, Geita, Tanaga, Mbeya, Mwanza kwa uchache wake.Tunatoa mikopo, kuzijengea uwezo taasisi za fedha na kutoa elimu ya masuala ya fedha,” alisema Bw. Mattaba ambaye pia alichukua nafasi hiyo kuwaomba watanzania kujitokeza kwenye maonesho ya uwekezaji.

Bw. Mattaba alisema wanufaika wakubwa wa mikopo ya Self ni wanawake, vijana na makundi maalumu na kwamba mfuko huo kupita NEEC utawafikia watanzania wengi na kufikia matarajio aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassani.

Naye Mkurugenzi wa Miradi wa Care Tanzania, Bi. Haika Mtui alisema shirika lake limekuwa likiunga mkono juhudi za serikali za kuwaondoa wananchi kwenye wimbi la umaskini na hasa kuwajengea uwezo.

“Tangu shirika lianzishwe mwaka 1994, zaidi ya wananchi 800,000 kati yao asilimia 70 ni wanawake. Tunaunga mkono juhudi za serikali katika kubadilisha maisha ya wanawake na vijana,” alisema na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zinazotolewa na NEEC kwa kushirikiana na wadau wake.

Kauli Mbiu ya Kongamano hilo la saba ni ‘Uwezeshaji kwa Uchumi Endelevu’ kwani inatoa fursa ya kujadili kwa kina masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa uchumi endelevu wa Tanzania.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la wezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Being’i Issa akijadili jambo na Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara na masoko wa mfuko wa Fedha wa SELF MF, Bw, Petro Mattaba (kushoto) na Mkurugenzi wa miradi wa Shirika la Care Tanzania, Bi. Haika Mtui (Kulia) mara baada ya kikao cha pamoja na waandishi wa habar kuelezea maandalizi na namna walivyojipanga kuelekea kongamano la Saba la uwezeshaji wananchi kiuchumi litakalofanyika tarehe 29 mwezi huu jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...