Wataalam wa Ardhi kutoka chuo kikuu cha Ardhi wameendesha Mafunzo ya kuwajengea ufahamu juu ya sheria na usic mamizi wa Ardhi kwa Madiwani wakuu wa idara na vitengo, maafisa wa watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na wawakilishi wa mabaraza ya ardhi wa vijiji vyenye migogoro.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo kikuu cha Ardhi Fredrick Magina amesema  kitendo cha Serikali ya kijiji kugawa Ardhi bila kuangalia mahitaji ya Wananchi, kutokuwa na Mipango ya matumizi ya Ardhi ya kijiji,kutokuwa na Uangalifu Katika kumiliki Ardhi  hivyo ni baadhi ya vyanzo  visababishi vya migogo ya ardhi.

Magina amesema lengo la mafunzo hayo kuwa ni kutoa Elimu kuhusiana na masuala yanayohusiana na  usimamizi wa Ardhi  kutokana na kuwepo kwa migogoro ya Ardhi hapa nchini.

Vilevile amesema  kutokana na Rasilimali zilizopo  ukilinganisha na Ongezeko la mahitaji ya watumiaji  hususani kwa upande wa Kibaha , wameona  ni vema kuchagua baadhi ya kata, madiwani, watendaji na wajumbe wa Baraza la Ardhi  Ili kuwapa Elimu juu ya usimamizi wa Sheria na za Ardhi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Erasto Makala amesema mafunzo hayo  yamekuwa mwanga wa kuwasaidia katika Kutoa usuluhishi wa masuala ya Ardhi.

Diwani wa Kata ya  Kwala Mansoor Kisebengo amesema Mafunzo hayo yamewasaidia kwenye mambo   ambayo walikuwa hawafanyi sasa wanaenda kuyafanya kwa kufuata sheria na kusaidia serikali kupambana na migogoro ya ardhi 

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Salma Mwalimu amesema  Mafunzo waliyoyapata kuhusiana na Ardhi yamewajengea uwezo wa kwenda kutatua migogoro katika sehemu zao za kazi na kuepuka kuzalisha migogoro mipya.








.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...