WAZAZI wameshauriwa kuwaelewa watoto wap kimaadili mazuri ili kuepukana na vishawishi na kuingia kwenye wimbo la mapenzi kwa kudanganywa kwa vitu vidogo kama Chipsi.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 9,2023 na    Mdau wa Maendeleo Bw. Ayubu Semvua katika mahafali ua shule ya msingi Turiani Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Bw. Semvua amesema ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha watoto wanaishi katika maadili mazuri kwani kunamjenga mtoto kukua kwa kutambua mema na mabaya.

Amesema malezi ya mtoto yanaanzia nyumba, hivyo wazazi wanajukumu la kusimamia mienendo ya watoto wao hasa kwenye masuala ya tabia ili kuepuka makundi hatarishi kwenye jamii inayotuzunguka.

Pamoja na hayo amewataka wahitimu kuepuka kujichanganya na makundi hatarishi ambayo yanaweza kusababisha kuingia kwenye vishawishi hatarishi.

Katika Mahafali hayo uongozi wa shule umempongeza mdau wa Maendeleo Iddy Azan kwa namna anavyochochea Maendeleo katika shule hiyo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...