Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa pongezi kwa Shirika la Madini la Taifa STAMICO kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi mazingira.
Ametoa pongezi hizo aliposhiriki zoezi la upandaji miti mkoani katika viwanja vya Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambapo amewshukuru kwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa Agosti 12, 2022 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa STAMICO.
Amesema kuwa shirika hilo lilikuja na Kampeni ya STAMICO na Mazingira at 50! kwa lengo la kuhakikisha pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini kuhakikisha mazingira yanatunzwa kikamilifu.
“Mtakumbuka nilifanya ziara ya kushtukiza kutembelea eneo la Ipagala (Dodoma) kuona kama kweli mmetekeleza kwa vitendo maelekezo, nimekuta kweli mmetekeleza yote kwani niliona mmezungushia uzio na miti inaendelea vizuri sana,” amesema Dkt. Jafo.
Pia, ameshukuru STAMICO kwa kufanya kazi kwa pamoja na vikundi mbalimbali vikiwemo Kikundi cha Wanawake na Samia ambapo walipewa kazi ya kazi ya kupanda na kutunza miti 560 eneo la EPZA ambayo inazidi kustawi.
Aidha, amewasifu kwa kuwapa uwakala ya kuuza nishati mbadala ya kupikia kwa Mkoa wa Geita, hatua itakayosaidia katika kuhifadhi mazingira kuepouka ukataji wa miti ovyo.
Katika
zoezi hilo jumla ya miti 340 ilipandwa pia na viongozi wengine akiwemo Waziri
wa Madini Mhe. Antony Mavunde, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Nyang’wale Grace Kingalame
pamoja na viongozi wengine.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti mkoani katika Viwanja vya
Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambako yanafanyika Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia
ya Madini leo Septemba 25, 2023.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akiwanawisha viongozi na wadau mara baada ya kushiriki katika zoezi la panda
mti katika Viwanja vya Bombambili (EPZA) mkoani Geita ambako yanafanyika
Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini leo Septemba 25, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...