Na Janeth Mesomapya

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuharakisha mchakato wa kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia nchini.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Septemba 20, 2023 pindi alipotembelea banda la PURA kwenye kongamano la nishati linaloendelea kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mnaongeza kasi katika mchakato wa kunadi vitalu vyetu ili wawekezaji waje kuwekeza katika utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini ili nchi inufaike,” aliongeza.

Akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni alieleza kuwa Mamlaka inaendelea na shughuli za awali za utekelezaji wa duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi kwa maeneo ya nchi kavu na baharini kwa lengo la kuongeza wawekezaji.

Aliongeza kuwa sambamba na maandalizi hayo PURA inaendelea kuweka mipaka ya vitalu vitakavyonadiwa na kuandaa vifurushi vya data (Data Packages) kwa kila kitalu.

“Hadi sasa vitalu 26 vinafanyiwa uchambuzi ili kupendekezwa kwa ajili ya kuingizwa katika mnada. Kati ya hivyo, vitalu 15 vipo nchi kavu na 11 vinapatikana baharini,” alifafanua Mhandisi Sangweni.

Alibainisha pia kuwa Serikali inatarajia kuzindua zoezi la kunadi Vitalu kati ya mwezi Desemba, 2023 hadi Machi, 2024 baada ya kukamilika kwa shughuli za maandalizi zinazoendelea.

Inaelezwa kuwa zoezi la kunadi vitalu linakadiriwa kugharimu jumla ya Shilingi bilioni 3.5. Aidha, kwa mwaka 2023/24 Serikali kupitia PURA imetenga Shilingi milioni 500 kwa ajili ya kazi za awali za maandalizi ya zoezi hilo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni kuhusu kuharakisha mchakato wa kunadi vitalu vya utafutaji mafuta na gesi asilia nchini. Ametoa maelekezo hayo Septemba 20, 2023 kwenye kongamano la nishati linaloendelea katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) Septemba 20, 2023 wakati wa kongamano la nishati linaloendelea katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Usimamizi wa Data kutoka PURA Bi. Rahma Ali akitoa maelezo ya vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia vinavyotarajiwa kunadiwa kwa moja wa washiriki wa kongamano la nishati waliotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.



Mjiofizikia wa PURA Josephine Jumanne akitoa maelezo kuhusu zoezi la kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa washiriki wa kongamano la nishati waliotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau kutoka PURA, Charles Nyangi akitoa maelezo kuhusu zoezi la kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa waandishi wa gazeti la Daily News wakati wa kongamano la nishati linaloendelea katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...