* Miradi 20 kupata ufadhili

KAMPUNI Ya Michezo wa kubashiri ya BetPawa Tanzania imezindua rasmi msimu wa pili wa kampeni ya 'Dream Maker's mahususi kwa kusaidia kutimiza ndoto za watanzania ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kupitia shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Afisa Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Jehud Ngolo amesema, katika msimu wa kwanza kampuni hiyo ilifadhili na kutimiza ndoto katika miradi 13 kwa gharama ya Shilingi milioni 200.

"Betpawa imesajiliwa na ina leseni ya kufanya biashara ya kubashiri ya kimtandao, niwapongoze kwa kutenga fungu kutoka katika mapato yao kwa shughuli za kijamii hususani kupitia programu hii bunifu na fursa kwa watanzania kutimiza ndoto zao kupitia BetPawa." Amesema.

Aidha amesema, kwa mujibu wa sheria asilimia 5 ya mapato yanayaotokana na michezo ya sheria yameeelezwa katika kuendeleza michezo na kampuni nyingine zimekuwa zikifadhili michezo mbalimbali ikiwemo kampuni hiyo ya BetPawa ambayo ina mkakati wa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF,) kwa kujenga uwanja wa michezo maalum kwa watu wenye ulemavu pamoja na kufadhili mchezo wa kikapu.

"Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini itaendelea kusimamia Sheria katika uendeshaji wa michezo hii pamoja na kuweka mazingira bora ya uendeshaji wa Biashara hii nchini... Niwapongoze BetPawa na kampuni nyingine ziige mfano huu." Ameeleza

Vilevile ametoa rai kwa watanzania kutotumia mchezo wa kubahatisha kama mbadala wa ajira bali waifanye kama sehemu ya burudani na kuepuka uraibu.


Kwa upande wake Meneja Masoko wa BetPawa Tanzania Borah Nganyungu amesema wamezindua kampeni hiyo ya Dream maker kwa lengo la kusaidia Jamii kupitia mawazo chanya watakayowasilisha.

Amesema, kampeni hiyo itahusisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ambapo jumla ya miradi 20 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 itafadhiliwa na BetPawa.

"Mafanikio yameongezeka na miradi pia imeongezeka zaidi BetPawa imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunarudisha kwa jamii kupitia njia mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya usalama kwa madereva bodaboda kwa kushirikiana na jeshi la Polisi pamoja na hili la kufanikisha ndoto za wananchi." Amesema.

Kuhusiana na namna ya kujisajili Borah ameeleza kuwa;

"Watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea watakaokutana na basi maalum la Dream Maker watakaribishwa kupanda na kujaza fomu au kurekodi video kuhusu ndoto zao. Wengine ambao hawatapata fursa ya kukutana na basi, wanaweza kufanya hivyo popote pale walipo na kutuma kwa njia ya mtandao kwa kutumia hastag #betPawaDreamMaker,” ameeleza.

Kwa mujibu wa BetPawa Tanzania, msimu wa kwanza wa Dream Maker uliofanyika Septemba 2021, uliwezesha ndoto za Watanzania 13 kutimizwa. Ndoto hizo ni pamoja na ujenzi wa nyumba mpya, viwanja vya michezo ufunguzi wa biashara mpya ambazo pia zimetengeneza ajira kwa jamii inayozizunguka. Mwaka huu, jumla ya miradi 20 itapata ufadhili.



Afisa Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Jehud Ngolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'Dream Maker's msimu wa pili mahususi kwa kusaidia kutimiza ndoto za watanzania kupitia mawazo yao bunifu na kuwataka watanzania kujitokeza ili kupata fursa ya ufadhili huo. Leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania Borah Nganyungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'Dream Maker's kwa msimu wa pili na kuwataka watanzania kueleza mawazo chanya ili wapate fursa ya ufadhili. Leo jijini Dar es Salaam.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...