Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Malenya amewataka mafundi wanaojenga miradi ya ujenzi katika wilaya ya Namtumbo kuzingatia michoro waliyopewa Ili kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo na  kuondoa maswali au sintofahamu zinazoweza kujitokeza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo.

Akiongea na mafundi ,kamati za ujenzi na viongozi wa Serikali katika ujenzi wa shule ya msingi mchomoro,shule mpya ya msingi masuguru pamoja na Shule ya Sekondari ya Dkt Samia Suluhu Hassan ,Malenya aliwasizitizia mafundi na viongozi wanaosimamia miradi hiyo kusimamia vipimo vilivyoko katika michoro na sio vinginevyo.

Malenya amefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi katika shule ya msingi Mchomoro, Masuguru pamoja na Sekondari ya Dkt Samia Suluhu Hassan  Kwa kujionea changamoto na Kisha kuzipatia ufumbuzi 
Ili kazi hizo za ujenzi ziweze kutekelezwa Kwa ufanisi mkubwa.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...