Na Mwandishi wetu

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesaini mkataba wa ushirikiano katika  udhibiti wa uchepushwaji wa  kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya, lengo likiwa ni kukabiliana na biashara haramu ya kemikali hatari.

Mkataba huo umehusisha Mamlaka ya Maabara ya Kemikali ya Serikali (GCLA), Mamlaka ya dawa na Vifaa Tiba ya Tanzania (TMDA), Baraza la Famasi la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), na wawakilishi kutoka sekta binafsi katika viwanda vya kemikali na dawa tiba zenye asili ya kulevya 

Tukio la utiwaji saini wa mkataba huo umefanyika leo Oktoba 16,  2023 katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Utalii cha Ngorongoro jijini Arusha.

Akizungumza  wakati wa utiaji Saini wa mkataba huo Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Aretas Lyimo amesema Kichocheo kikuu cha kuimarisha juhudi hizi za pamoja kupitia mkataba huo wa ushirikiano ni uwepo wa viashiria vinavyoonyesha ongezeko la biashara haramu ya kemikali hatari na matumizi yake katika uzalishaji wa dawa ya kulevya na dawa mbadala ya kulevya.

"Mkataba huu wa ushirikiano tunaangalia sehemu zenye uchepushwaji mkubwa wa dawa,   tulishafanya kwa wadau wa  Dar es  salaam na leo Arusha na tutaangalia miji mingine yenye tatizo kama hili nako  tutafanya na baadaye tutaunda umoja wa wauzaji wa kemikali bashirifu na famasi zenye kibali cha kuuza dawa tiba zenye asili ya kulevya...

" Ili kuhakikisha tunawekeana utaratibu wa kufuatiliaji wa karibu kuhakikisha tunazuia uchepushwaji wa kemikali bashirfu na dawa tiba zenye asili ya kulevya, "amesema Kamishna Jenerali  Aretas Lyimo.

Kwa upande wake Meneja Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kaskazini Eliamni Mkenga amesema Maabara hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu wa DCEA kwa kuwa wanashirikiana nao kwa kiasi kikubwa udhibiti wa uchepushwaji wa kemikali bashirifu na udhibiti wa dawa zingine za kulevya.

‘’Kwenye dawa za kulevya tuna maeneo mawili makuuu tunayoshirikiano na Mamlaka.Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanya kazi ya uchuguzi wa dawa za kulevya ikisaidiana na polisi pamoja na kitengo maalumu cha udhibiti wa dawa za kulevya.

"Lakini baada ya kuanzishwa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya tunashirikiana nao katika kutambua aina za dawa za kulevya na kupima watumiaji kujua aina ya dawa za kulevya  wanazotumia.

" Pia Maabara ya Nkemia Mkuu wa Serikali inangalia kemikali bashirifu na kwa kawaida inabidi kila mwezi inabidi tuwe na wasilisha ni kemikali gani  zinapatikana nchini lakini mwisho kabisa tunatoa Ushahidi mahakamani kwa kitaalamu’’ amesema.

Wakati huo huo Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ya Tanzania (TMDA) Kanda ya Kaskazini Proches Patrick amesema watatoa ushirikiano mzuri kwa mamlaka na taasisi zote zilizoingia makubaliano ya ushirikiano huo.

‘’TMDA), itaendelea kushirikiana na DCEA pamoja na taasisi zote ambazo zimeingia kwenye makubaliano haya tunashirikiana na utekelezaji wake unakuwa na tija."

Kwa upande wa wadau wa kutoka sekta binafsi katika viwanda vya kemikali na dawa tiba zenye asili ya kulevya wasema ushirikiano huo ni muhimu katika kuwasaidia wananchi wasipate madhara yanayotokana na dawa za kulevya zinatokana na kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.

Pamoja na hayo imeelezwa mkataba wa ushirikiano huo unawakilisha hatua muhimu katika jitihada za kudhibiti kuenea kwa vitu hatari nchini Tanzania kinyume cha sheria






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...