Na Mwandishi Wetu, Mwanza.

SHIRIKA la usimamizi wa mazingira na maendeleo (EMEDO) la Mwanza Nchini Tanzania kwa ushirikiano na Shirika la Wanaharakati wa Ubuntu wa mazingira nchini Kenya (NAAM Festival) wamezindua mradi maalum wa Sanaa unaoitwa "Sanaa Ziwani Nyanza", mradi utakaokuwa wa mafunzo na sanaa ya maonesho.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka NAAM Festival, Mradi huo unalenga kujenga ushirikiano kati ya wasanii na wadau wa sanaa, katika kuongeza ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya kijamii katika tasnia ya Sanaa.

"Mradi huu unazinduliwa leo tarehe17, Oktoba 2023, kupitia warsha ya siku 10 ambayo inafanyika katika ofisi za EMEDO jijini hapa.

Wasanii 6, wanashiriki kwenye warsha hii, Lakini pia utaambatana na maonesho ya Sanaa 'Art exhibition' ambayo yatafanyika tarehe 28 Oktoba 2023." Imebainisha taarifa hiyo ya NAAM Festival.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa, Mradi huo unaungwa mkono na Taasisi ya Nafasi Art Space kupitia msaada wa Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania, pamoja na Ubalozi wa Norway.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...