Na Jane Edward, Arusha

Naibu waziri wa kilimo David Silinde amesema kilimo kina mchango mkubwa sana katika pato la Taifa ambapo kinaajiri zaidi ya asilimia 65.6 na kuchangia pato la Taifa kwa asimilia 26.1 .

Akizungumza katika  hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi kutoka shirika la kilimo na chakula Duniani (FAO) na kuipatia mamlaka ya afya ya mimea na viwatilifu Tanzania (TPHPA)kutoka mradi wa STREPHIT unaosimamiwa na FAO ambapo vifaa hivyo ni utekelezaji wa mradi wa kuimarisha huduma za afya ya mimea kwa usalama wa chakula nchini ambapo kiasi cha Bilion 2.2 zimetumika.

Amesema kilimo kinachangia mapato yatokanayo na mauzo ya nje kwa USD bilion 1.2 sawa na asilimia 20 ya mauzo ya nje kwa mwaka .

Aidha mradi huo wa STREPHIT nimradi wa miaka 3 na nusu ambao unalenga kutatua mapungufu ya uendeshaji na kiufundi yanayohusiana na afya ya mimea ambapo una mchango mkubwa  katika pato la Taifa na utaajiri zaidi ya asilimia 65.6 na kuchangia pato la Taifa kwa asimilia 26.1

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa TPHPA Profesa Joseph Ndunguru amesema vifaa hivyo vitakuwa mchango mkubwa sana katika kutekeleza majukumu ya mamlaka hiyo sambamba na kuongeza ufanisi na shughuli za mamlaka hiyo na kudhibiti viwatilifu na kuongezeka kwa uhakika wa chakula na malighafi ya viwanda.

Amevitaja vifaa walivyopokea kutoka FAO magari 7 land cruiser,, pikipiki 19 ,ndege nyuki 20,vishikwambi 41 ,, min lab inspection tables17, friji 17,kompyuta 34 ,, wife routers 17, Ethernet switch 17 na illuminated magnifier 17 vyenye thamani ya shilling bilion 2 .2.

Ndunguru amesema utekelezaji wa shughuli hizo za mamlaka unalenga kuongeza tija kwenye mnyororo wa thamani wa mazao na viuatilifu na hatimaye kuinua sekta ya kilimo na uchangiaji kwenye pato la Taifa kama ilivyo ainishwa kwenye agenda 10/30 inayolenga kukuza kilimo kwa asilimia 10 ifikapo 2030.

Aidha ameishukuru Wizara ya kilimo kwa kyanzisha mradi huo ,washirika wa maendeleo wa jumuiya ya umoja wa ulaya (EU)kwa kutoa rasilimali fedha vitendea kazi ambapo FAO imeratibu na kutoa utaalamu kupitia Tanzania kupitia mradi huo .

Naibu Waziri wa kilimo David Silinde akijaribu kuwasha pikipiki katika hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi kutoka shirika la FAO .

 Profesa Joseph Ndunguru ambaye ni kaimu mkurugenzi wa TPHPA akipeana mkono na mwakilishi wa FAO mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...