
Mkuu wa Idara ya Upasuaji Dkt. Eric Muhumba amesema upasuaji huo utafanywa na wataalamu wa MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa kupunguza uzito na Upasuaji Rekebishi kutoka India, Dkt. Mohit Bhandari.
Dkt. Muhumba ameongeza kuwa huduma hizo za kupunguza uzito zinafanyika kwa kupunguza nafasi ya kuhifadhi chakula kwa kushona sehemu ya eneo la tumbo kitu kitakachosababisha mtu kutumia kiasi kidogo cha chakula hivyo kupunguza uzito.
Dkt. Muhumba amebainisha kuwa katika kutoa huduma hizo watatumia njia ya kisasa ambayo haitahusisha upasuaji ambapo watatumia kifaa maalumu kiitwacho endoskopia kuingia katika tumbo na kupunguza nafasi ya tumbo la chakula.
“Upasuaji huu utafanyika kwa bei nafuu sana ukilinganisha na endapo mtu angeenda kutafuta huduma hizi nje ya nchi, hivyo tumeamua kuwasogezea wananchi huduma hizi na kuwapunguzia usumbufu wa wananchi kusafiri nje ya nchi kutafuta huduma hizi”Amesema Dkt. Muhumba
Sambamba na huduma hizo Dkt. Muhumba ameongeza kuwa huduma rekebishi itahusisha kurekebisha kwa kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu ya mwili mfano kupunguza au kuongeza ukubwa wa matiti, nyama kwenye mikono na sehemu nyingine mbalimbali za mwili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...