Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
Oct 11

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete ambae pia alikuwa mbunge wa kwanza jimbo la Chalinze amesema, uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Biteko sio jambo la kushangaza kwani ni Naibu Waziri Mkuu wa tatu sasa.

Amesema ,Rais Samia Suluhu Hassan amefanya chaguo sahihi ,katumia Mamlaka yake ya kikatiba.

Kikwete aliyaeleza hayo, wakati wa mkutano maalum wa jimbo la Chalinze kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2023, ambayo ilitolewa na mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete.

Kikwete anasema Naibu Waziri Mkuu wa kwanza alikuwa Salim Ahmed Salim ,Wa pili Agustino Mrema na wa tatu ni Dkt.Dotto Biteko.

"Ni hakika ni chaguo zuri ,midomo imeumbiwa kusema,wapo wanaosema, kuwa Rais kavunja katiba hakuna katiba iliyovunjwa kwa kuwa hakuongeza Waziri Mkuu wapili ila kateuwa Naibu Waziri Mkuu"

"Biteko fanyakazi zako,kwa mujibu wa katiba ya nchi,mwenye Mamlaka ya kufanya maamuzi ni Rais,usitetereke, "Rais katumia Mamlaka yake ya kikatiba,midomo imeumbiwa kusema,waache waseme fanya kazi"alisisitiza Kikwete.

Kikwete pia aliwataka viongozi waCCM kufanya kazi na kusimamia Chama ili kupata ushindi uchaguzi ujao 2024/2025.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ,Dotto Biteko alitoa rai kwa wanaCCM kufanya siasa za kubadilisha maisha ya watanzania katika kuwaletea maendeleo badala ya kufanya siasa za maneno matupu zisizojibu hoja.

Aidha aliwaasa watumishi wa Umma kuwahudumia wananchi na kuwafuata walipo pasipo kuwasubiria walete kero zao kwenye madawati.

"Wapo wanaojaribu kutusi na kukejeli,nyie wapeni muda msiwajibu ,msiingie kwenye matusi na kejeli wajibuni kwa hoja na Mambo makubwa yanayofanywa na Serikali na Chama Chetu"alisisitiza Biteko.


Hata hivyo ,Biteko alisema ameridhishwa na namna halmashauri ya Chalinze inavyosimamia fedha za miradi.


"Mafanikio haya ni dhahiri kwamba , umoja wenu ushirikiano na upendo ndio ushindi huu unaoonekana leo, Makusanyo ya Bilioni 15 katika halmashauri moja ni kazi kubwa ya mbunge kusimamia na kuwa na watendaji na madiwani kwa umoja "


RIDHIWANI KIKWETE


Akielezea utekelezaji wa ilani 2020-2023 , mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,anasema utekelezaji umefikia asilimia 96 ,na sasa hatua waliyofikia inawabeba kutembea kifua mbele.


Kuhusu sekta ya maji ,alieleza awali kulikuwa na asilimia 62 inayofikisha huduma ya maji kwa wananchi lakini sasa imefikia asilimia 96 ya upatikanaji maji.


"Tunaishukuru Serikali kwa kutenga Bilioni 1.4 kupeleka fedha kwa ajili ya maji Kibindu'"


Alisema, wakati anaingia madarakani zilizalishwa lita milioni 7.2 na kuhudumia wateja 3,236 ambapo sasa imefikia lita milioni 7.2 zinazohudumia wateja 7,500 huku kukiwa na vioski 1,224 kutoka 114 vya awali.


Akielezea kuhusiana na nishati ya umeme ,vijiji vyote 75 vimefikiwa na umeme na kata zote 15 kilichobakia ni hatua ya uunganishaji umeme kwa wananchi.


"Naliomba Shirika la Umeme Tanesco, na REA kuongeza nguvu ili kuweza kuwafikia wananchi kuwaunganishia na kusambaza umeme"alisema Ridhiwani.


Ridhiwani alieleza nishati ya umeme shule za msingi 108 zimeunganishwa umeme.


Kikwete alisema, tayari sh. Biln sita zimepokelewa katika Halmashauri ya Chalinze kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo na kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali.


Kuhusu Elimu Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliishukuru Serikali wakati anaingia katika nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo kulikuwa na shule za Sekondari 17 na sasa zimefikia 25 ikiwa ni ongezeko la shule nane.


Alibainisha, ujenzi wa shule za msingi umeongezeka na kuondoa kikwazo cha mlundikano wa wanafunzi darasani na sasa kufikia 113.


Vilevile Ridhiwani alieleza kuwa, ameshatembelea kata zote na vijiji vyote kukutana na wananchi kujua kero zao na kujua namna ya kuendelea kuzitatua.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...