Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMIA ya raia wa China waishio nchini Tanzania wakiongozwa na Balozi wa China nchini Chen Mingjian wamehudhuria Tamasha la China la Mid-Autumn lililokwenda sambamba na kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa BRI huku Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro akitumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa China kuendelea kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya michezo.

Wakati wa tamasha hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam raia hao wa China wamepata nafasi ya kushuhudia buradani kutoka vikundi vya muziki wa asili vya Tanzania na China huku pia Dk.Ndumbaro akielezea kwa kina urafiki na uhusiano wa nchi hizo mbili ulivyowezesha kupatikana kwa mafanikio makubwa.

Pamoja na hayo pia Dk.Ndumbaro ametoa rai kwa raia wa China kuja kuwekeza nchini kwa kujenga miundombinu mbalimbali hasa katika kipindi hiki ambacho nchi za Tanzania, Kenya na Uganda wamepata nafasi ya kuandaa michuano ya AFCON itakayofanyika mwaka 2027.

"Tunawaalika wawekezaji kutoka nchi ya China kuja kuwekeza nchini Tanzania katika maeneo mbalimbali hasa yanayohusu sekta ya michezo, kama mnavayofahamu Tanzania, Kenya na Uganda tutakuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON.

Pia Dk.Ndumbaro ameiomba Serikali ya China kusaidia Tanzania katika ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya utamaduni, sanaa na michezo hasa katika Mji wa Dodoma. "Tanzania tuna uhaba wa miundombinu ya kitamaduni hasa katika mji mkuu mpya wa Serikali Dodoma.

" Kutokana na uhaba huo tunaiomba Serikali ya China pia kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo mradi wa nyumba ya Kitaifa ya Utamaduni ulioanzishwa na Serikali ya Tanzania kwa madhumuni ya kuonyesha utambulisho wa Mtanzania na shughuli zote za kitamaduni chini ya paa moja, " amesema Dk.Ndumbaro.

Kuhusu uhusiano wa Tanzania na China, Dk.Ndumbaro amesema nchi hizo zimekuwa na ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu ambao umesaidia kuwepo kwa mafanikio makubwa katika nyanja zote.

"TunafahamuTanzania ilisaini mkataba wa kitamaduni na Serikali ya China Aprili 30, 1992 na kuendelea kufufua programu mbili za utekelezaji (2017-2020) na (2022-2025) kwa upande wa Utamaduni na Sanaa."

Amesisitiza ushirikiano huo umeendelea kuimarika kutokana na utoaji wa fursa mbalimbali za mafunzo, kubadilishana uzoefu na ujuzi wa masuala ya utamaduni na sanaa ambao umetolewa na Serikali ya China kwa Watanzania.

Aidha amesema Serikali zote mbili zimeshirikiana na katika matukio tofauti ya kitamaduni kama vile semina ya usimamizi wa michezo ya kuigiza kwa nchi za Afrika zilizofanyika Aprili 24 hadi Mei 4, 2019 iliyotolewa kwa maofisa wa Wizara walioshiriki katika semina hiyo iliratibiwa na Chuo Kikuu cha Taaluma cha Utawala wa Utamaduni na Utalii (CACTA) huko Beijing, Uchina.

Ameongeza mwaka 2020 China imetoa semina za mtandaoni kwa wataalam na wasimamizi wa utamaduni kuhusu maendeleo jumuishi ya sekta ya utamaduni na utalii ya Kitaifa...

Huku pia akielezea fursa kwa Wachina wengi zaidi kujifunza Kiswahili na Watanzania kujifunza lugha ya Kichina kwa kuzingatia kwamba lugha ni nyenzo muhimu ya mawasiliano na kukuza biashara na shughuli zote miongoni mwa watu wa nchi hizo mbili.

Awali Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Chen Mingjian amesema pamoja na mambo mengine mwaka huu ni umuhimu na wakipekee katika uhusiano kati ya China na Afrika, ila kubwa zaidi ni uhusiano uliopo kati ya China na Tanzania.

Amefafanua pia mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 10 ya pendekezo la Rais Xi Jinping la mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja."

Balozi Chen amesema miaka 10 iliyopita, chini ya mwongozo wa diplomasia kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, mpango wa "Ukanda mmoja na Njia moja" na dhana ya uaminifu, matokeo ya kweli, mshikamano na imani nzuri katika kushughulikia Afrika, urafiki kati ya China na Tanzania umekuwa.

"Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeendelea kuimarika, na ushirikiano wa kiutendaji umekuwa na matokeo yenye tija.Idadi kubwa ya Wachina wa ng'ambo nchini Tanzania wote ni mashahidi na walengwa pia ni washiriki na waendelezaji,"amesisitiza Mingjian.

Aidha katika katika siku zijazo, anatumaini kuwa marafiki wote wa China walio nje wanaweza kujumuika kikamilifu katika mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kivitendo sambamba na kupata maendeleo yao wenyewe, na kuendelea kuunda sura mpya ya urafiki kati yao.


Akizungumzia Tamasha la Mid-Autumn amesema ni Sikukuu muhimu ya kitamaduni kwa watu wa China na familia zao. "Siku ya muungano.


“Ninawakumbuka zaidi wapendwa wangu wakati wa msimu wa sherehe.” Tunahisi hivyo kwa undani zaidi tunapokuwa katika nchi ya kigeni. Katika miaka michache iliyopita, tumepitia mtihani wa janga la Covid-19 kwa pamoja."

Aidha amesema tamasha hilo ni la kwanza kubwa kufanywa na Wachina wa nje ya China tangu janga hilo na anaamini kila mtu amekuwa akitazamia tukio la kupendeza lililopotea kwa muda mrefu. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za pekee kwa Chama Kikuu cha Wafanyabiashara wa China, Chama cha Wakandarasi wa Kichina na vikundi vingine vya wachina vya ng'ambo, vyama vya wafanyabiashara na wafanyabiashara kwa juhudi zao katika kukuza utendaji huo.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian(kushoto) akisalimiana na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro (kulia)wakati wa hafla ya Tamasha la China sambamba na Sherehe za Miaka 10 ya BRI.Tamasha hilo limehudhuriwa na mamia ya raia wa China waishio nchini TanzaniBalozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian(kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro (kulia)wakati wa hafla ya Tamasha la China sambamba na Sherehe za Miaka 10 ya BRI.Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akizungumza wakati wa Tamasha hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam.Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro.Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian(katikati) akipiga makofi kufurahia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro wakati wa hafla ya Tamasha la China sambamba na kusherehekea Miaka 10 ya BRI.Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Thomas Mihayo(katikati) akipiga makofi wakati wa tamasha hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...