Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya mwisho ya Promosheni ya Maokoto Deilee inayoratibiwa na Sportpesa kushirikiana na mtandao wa Tigo imefanyika leo terehe 10, Oktoba 2023 jijini Dar es Salaam, na amepatikana mshindi mmoja wa jumla wa kitita cha shilingi Milioni 15/-.

Mshindi wa kiasi hicho cha fedha ni Diatus Ishengoma kutoka mkoani Arusha ameshinda kitita hicho cha shilingi Milioni 15/- kupitia promosheni hiyo ya Maokoto Deilee.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Sportpesa kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Lydia Solomon amewashukuru wateja wote walioshiriki kucheza promosheni hiyo sanjari na mtandao wa Tigo ambao wameshirikiana nao muda wote.

Lydia amesema washindi takribani 571 wameshinda na kuzawadiwa zawadi mbalimbali kupitia promosheni hiyo kwenye droo zake ambazo zilichezeshwa sehemu mbalimbali ikiwa kwenye Ofisi za Sportpesa.

Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Tigopesa, Fabian Felician amesema zaidi ya Washindi 571 wameshinda zawadi mbalimbali kupitia Tigopesa, amesema fedha hizo zitawasaidia kubadilisha maisha

Vile vile, kupitia droo hiyo ya mwisho amepatikana Mshindi wa shilingi Milioni moja ambaye ametoka mkoa wa Iringa

wakati Washindi wengine wawili wa Simu janja, mmoja ametoka Dar es Salaam na mwingine ametoka mkoa wa Morogoro.

Katika promosheni hiyo ya Maokoto Deilee ambayo ilianza tarehe 21 Agosti, 2023, washindi wote ni zaidi ya 571 wamepatikana katika siku 50 za promosheni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...