MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametimiza ahadi yake kwa kukabidhi matofali 300 yenye thamani ya Sh 450,000 ikiwa ni kuunga mkono ujenzi wa kanisa jipya la Parokia ya Ikungi.

Akikabidhi matofali hayo Octoba 9,2023,Katibu wa Mbunge Ally Rehani amesema ameagizwa kupeleka mchango huo kama ambavyo kanisa lilimshirikisha mbunge juu ya ujenzi huo.

"Nimekuja hapa kwa maelekezo ya Mbunge Mtaturu ili niwaletee mchango wake kwa ajili ya ujenzi huu wa Kanisa jQipya kama ambavyo mlimshirikisha,

"Mbunge Mtaturu anasema yupo pamoja nanyi kwa kila hatua na amewaomba kwa imani zenu muendelee kuliombea amani Taifa kwani bila amani hakuna maendeleo yatakayofanyika,".amesema Katibu huyo.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Kanisa Paroko Padre Vincent Alute amemshukuru sana mbunge kwa kutimiza ahadi yake na kusema siku zote amekuwa ni baraka kwenye kanisa na wananchi wa jimbo hilo.

"Tufikishie shukrani zetu,mwambie tunamuombea baraka nyingi sana,huu mchango utatusogeza mbali ili kuyafikia malengo ya kulijenga kanisa letu,".Ameshukuru Padre Alute.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...