Jumatatu, Oktoba 16, 2023 Ruangwa
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Sophia Mjema, amefunga mafunzo ya Falsafa, Itikadi na Sera za CCM kwa viongozi wa Chama na jumuiya zake mkoani Lindi.
Hitimisho la mafunzo hayo limefanyika katika wilaya ya Ruangwa mkoani humo.
Ndg. Mjema amewataka viongozi na wanachama wa CCM kuona fahari kuwa ndani ya CCM, kwani maendeleo makubwa yanayoonekana ni kazi kubwa inayofanywa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema, kwa kipindi kifupi kiongozi Mkuu wa nchi, ameonyesha umahiri na umadhubuti katika uongozi ndani na nje ya taifa la Tanzania.
Akizungumzia umuhimu wa mafunzo, alisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha viongozi wanakuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro na kuleta suluhu kwa kila changamoto inayowakabili wananchi.
"Nendeni mkabadilike na kuwa mfano kwa kukitumikia Chama kwa weledi na uadilifu, kiongozi lazima uwe safi lazima uwe wa mfano.
Hiki Chama ni chama cha wanyonge, kila mtu ana wajibu wa kuwa kiongozi wa mfano mzuri kimaadili," amesema Ndg. Mjema.
Amekemea baadhi ya vitendo vya ukiukwaji wa maadili vinavyosababisha wananchi kuonewa na kukosa haki.
Ndg. Mjema ametoa mfano wa migogoro ya ardhi kwamba baadhi ya viongozi wamekuwa ni sehemu ya kuwakandamiza wanaodhulumiwa ardhi zao.
Ndg. Mjema amewasihi viongozi kuwa daraja na kiungo katika kuimarisha umoja na mshikamano ili maendeleo yapatikane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...