Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile ameipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kuendelea kusimamia na kuendesha viwanja vya ndege hali iliyochangia kuongezea ya ndege yanayotoa huduma katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Menejimenti ya TAA, Naibu Waziri Kihenzile amesema Usimamizi huo umefanya miradi ya maboresho ya inayotekelezwa kwenda kasi na kukamilika kwa wakati.

“Hongereni kwa kazi nzuri mnayoifanya hasa kwenye usimamizi wa viwanaj na miradi inayoendelea, sasa juhudi hizi mzielekeze kwenye miradi iliyopangwa kwa mwaka huu wa fedha ili ikamilike kwa wakati na tuone thamani ya fedha’ amesema Naibu Waziri Kihenzile.

Naibu Waziri Kihenzile ameitaka TAA kuhakikisha Viwanja vya Ndege vya Arusha na Iringa vinawekwa taa ili kuviwezesha kutumika saa 24 na kukuza uchumi wa kanda hizo.

Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wa Taasisi za Uchukuzi kuhakikisha vibarua wanaofanya kazi kwenye miradi wanalipwa kwa wakati na kwa viwango ili kutokwamisha miradi hiyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA Mussa Mbura amemuhakikishia Naibu Waziri Kihenzile kuwa TAA kupitia idara ya Miundombinu itahakikisha inaongeza nguvu kwenye usimamizi ili kuhakikisha thamani inaonekana na stahili za vibarua zinalipwa kwa wakati.

Mbura ameongeza kuwa kwa sasa kupitia kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere safari za ndege zimeendelea kuongezeka kwa asilimia 29, abiria asilimia 50 na tani zimeongezeka kwa asilimia 15.

Naibu Waziri Kihenzile yuko katika ziara ya siku 5 jijini Dar es Salaam ya kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi hizo pamoja na kuzungumza na manejimenti za taasisi hizo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) alipofika kujitambulisha pamoja na kutaka kujua kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile alipofika kuzungumza na  Menejimenti ya TAA katika ukumbi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria TAA Pamela Mugarula akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile kuhusu kazi zinazofanywa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) alipofika kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kuzungumza na Menejimenti ya TAA katika ukumbi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakisikiliza hotuba ya  Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile alipokuwa anazungumza na Menejimenti ya TAA katika ukumbi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile (katikati waliosimama mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya TAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mussa Mbura( wa pili kushoto waliosimama mbele) mara baada ya kufanya mazungumzo na Menejimenti hiyo  katika ukumbi wa Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...