*Kutangaza Injili na kutoa huduma kwa jamii

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mwimbaji wa Njimbo za Injili wa Halisi Ministry Rehema Simfukwe kufanya ziara (Halisi Tour 2023) katika mikoa ya Dodoma na Arusha.

Ziara hiyo itafanyika katika kwa Mkoa wa Dodoma itafanyika Oktoba 12 na Arusha Itafanyika Oktoba 19 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Rehema amesema baada ya kutoa albam kwa miaka mitatu hivyo sasa anakwenda kutoa katika ziara katika kutoa huduma kwa jamii wamaeneo hayo na mikoa ya jirani.

Amesema katika ziara hiyo atatapita vyuo kuzungumza na wasichana kusema njia alizopita hadi kufika hapo na wao wawe chachu ya kufanya vizuri katika ndoto zao za maisha.

Simfukwe amesema ziara hiyo watachangisha fedha ya kusaidia watoto wenye vichwa vikubwa kuwasaidia Bima ya afya kwani watoto hao ni sehemu ya jamii.

Hata hivyo amesema ziara hiyo itakwenda kupambwa na  na wasanii wa Injili akiwemo Victor Maestro ili waweze kutoa huduma ya Mungu.

"Ndoto yangu imetimia kufanya ziara katika mikoa hiyo ni ya kuanzia tu na tutaendelea mikoa mingine kwa malengo yale yale" Amesema Rehema.

Rehema amebanisha katika nyakati hizi mambo mengi hayako sawa hivyo kunahitaji wenye maono ya Mungu kutoa huduma katika kuiweka sawa jamii.

Mwimbaji wa Njili wa Halisi Ministry Rehema Simfukwe akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake katika mikoa ya Dodoma , Arusha jijini Dar es Salaam. 

Mwimbaji wa Njili wa Halisi Ministry Rehema Simfukwe akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake katika mikoa ya Dodoma , Arusha jijini Dar es Salaam.

Mwimbaji wa Injili , Rehema Simfukwe na Victor Maestro wakionyesha umahiri wa kuimba jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Halisi Tour 2023  Heriel Mduma akizungumza kuhusiana na ziara ya Rehema Simfukwe katika mikoa ya Dodoma na Arusha , jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...