Na Mwandishi Wetu, WMNN.

SERIKALI ya Saudi Arabia imeipongeza Tanzania kwa kuimarisha amani na usalama na pia kupenda wageni wanaoingia nchini kutoka mataifa mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi mpya wa Saudia Arabia nchini, Yahya Ahmed Okeish, wakati alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 5, 2023.

Balozi huyo aliyeingia nchini mwezi uliopita, amesema anafurahishwa na usalama wa Tanzania na pia nchi yake ina ushirikiano mzuri na wahistoria wa miaka mingi na nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano na kusaidia katika shughuli mbalimbali ya kijamii na maendeleo kwa ujumla.

“Mheshimiwa Waziri nina furaha kuja kuonana na wewe, nimefurahishwa na usalama wa Tanzania, na pia ukarimu wenu wa kupenda wageni waliopo na wanaoingia nchini,” alisema Balozi Okeish.

Pia alisema Serikali ya Saudi Arabia itaendelea kutoa misaada nchini na wana vituo vinavyotoa huduma mbalimbali zinazosaidia kuleta maendeleo nchini, hivyo kupitia uhusiano wa kihistoria kati ya Saudi Arabia wataendelea kutoa huduma pale zitakapohitajika.

Kwa upande wake, Waziri Masauni pia aliipongeza nchi ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wake mkubwa kwa Tanzania, na kumkaribisha Balozi huyo kufurahia mambo mazuri yote yaliyopo nchini ikiwemo kujifunza masauala ya utamaduni.

“Mheshimiwa Balozi, nakubaliana na wewe nchi hizi mbili zina ushirikiano mkubwa na pia wa kihistoria, nakukaribisha sana Tanzania, na utajifunza mambo mengi ikiwemo kuhusu utamaduni wetu, pia tunawakaribisha wawekezaji kutoka Saudi Arabia waje nchini kwa kuwa nchi yetu ni salama,” alisema Masauni.

Waziri Masauni alisema Tanzania itaendelea kushirikiana na Saudi Arabia na pia itaendelea kudumisha amani ambayo iliyopo nchini, na pia aliishukuru Serikali ya Saudi Arabia kwa misaada mbalimbali ya maendeleo wanayoitoa nchini.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akizungumza na Balozi mpya wa Saudia Arabia nchini, Yahya Ahmed Okeish kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Saudi Arabia. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 5, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Balozi mpya wa Saudia Arabia nchini, Yahya Ahmed Okeish alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Saudi Arabia katika Kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 5, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Saudi Arabia Nchini, Yahya Ahmed Okeish, baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Saudi Arabia katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 5, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...