Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Tuzo ya Hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2023(Africa’s Leading National Park 2023) ikiwa ni mara ya tano mfululizo kushinda Tuzo hii baada ya kuwagaragaza  washindani wa tuzo hii  kama Central Kalahari Game Reserve- Botwswana,  Etosha National Park -Namibia,  Kidepo Valley National Park -Uganda, Kruger National Park -South Africa, mapoja na Masai Mara National Reserve - Kenya

Tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ usiku wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika hotel ya  _Atlantis The Royal Dubai  _ katika nchi za Falme za Kiarabu na kupokelewa  na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai, kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA)


.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...