SERIKALI imejipanga kuanzisha mtandao wa vijana nchini kwa lengo la kuwawezesha ili kuwanyanyua na wapige hatua za kimaendeleo.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na watu wenye ulemavu, mhandisi Cyprian Luhemeja ameyasema hayo mjini Babati Mkoani Manyara, kwenye mdahalo wa vijana katika mwendelezo wa wiki ya vijana kitaifa.

Mhandisi Luhemeja amesema serikali itaanzisha mtandao huo kupitia wilaya na mikoa mbalimbali ili kuwatamhua na kuwawezesha.

"Kuna baadhi ya mabenki nchini yanatoa mikopo kwa vijana mbalimbali bila kuwa na riba, bila kuwa na mtandao wa vijana wasiotambulika huwezi kuwafikia wote," amesema mhandisi Luhemeja.

Hata hivyo, amewataka vijana nchini kutambua kuwa Tanzania ndiyo nchi yenye fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kuwasaidia.

"Moja ya nchi pekee ukiamua kutoka unatoka kijana na kwenye wiki ya vijana kitaifa ya mwaka ujao tutawaita mawaziri wote wa kisekta ili watoe majawabu kwa vijana," amesema.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Chris Mauki amesema vijana wengi wamepoteza uaminifu hadi kusababisha kukosa fursa mbalimbali.

"Vijana hawaaminiwi tena kama awali mnapaswa kujitafakari kwa nini hamuaminiki pia marafiki zako Wana mchango mkubwa kwenye mafanikio yako," amesema Mauki.

Kijana wa kutoka Arusha, Mary Aloyce amesema vijana wengi hawajitambui kuwa ni viongozi wa leo kwani hata mikutano ya kijiji hawashiriki maamuzi na kulaumu hawashirikishwi.

Kijana wa mjini Babati, Grace Peter amesema kupitia mdahalo huo amejifunza umuhimu wa kutumia mitandao kwa faida na siyo kujiburudisha pekee.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...