SERIKALI Imepongeza Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO,) kwa kutekeleza kwa vitendo malengo ya Nchi katika sekta ya Elimu kwa kuleta ujuzi kwa watoto.

Hayo yameeelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati alipotembele Banda la Taasisi hiyo na kufunga Kongamano la maadhimisho ya Kitaifa la Juma la Elimu kwa Watu Wazima lililohitimishwa mwishoni mwa wiki Kibaha mkoani Pwani.

Prof. Mkenda amesema, Taasisi hiyo kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC's,) imekuwa ikitoa ujuzi pamoja na elimu kwa makundi mbalimbali na kukuza uchumi kupitia mafunzo yanayotolewa kupitia vyuo hivyo.

Amesema, Serikali inatambua jitihada hizo na wamekuwa wakishiriki na wadau wa namna hiyo katika kuendeleza Elimu ya Watu Wazima katika kusaidia jamii kukabiliana changamoto zilizopo.

Prof. Mkenda amesema, program zinazotekelezwa za Elimu Msingi kwa walioikosa (MEMKWA,) Mpango wa Elimu Changamani kwa Walio nje ya Shule (IPOSA,)  na Mpango wa Elimu kwa njia Mbadala (AEP,) kutaongeza tija na kuwajengea uwezo vijana na watu wazima katika kuchangia uchumi endelevu na kuboresha maisha yao.

Akiwa katika Banda la KTO Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo ya amali ambayo yanatija kwa jamii.

"KTO endeleeni na ushirikiano huu wa kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na elimu...mafunzo ya amali yana tija kwa jamii ya sasa tunaona kupitia mafunzo mnayotoa vijana wanajiajiri na kuajiri wengine." Amesema.

Pia Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amesema kuwa, KTO kupitia Vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC's) vinavyopatikana kote nchini vinatekeleza lengo la nchi katika sekta ya elimu ambalo ni kuleta ujuzi kwa watoto na makundi mengine wakiwemo vijana.

Dkt. Msonde amesema, msingi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi ni kutoa ujuzi ili wanufaika waweze kujitegemea na kuwataka kutanua wigo zaidi wa kutoa mafunzo hayo kwa wote bila kuangalia elimu bali watoe ujuzi utakaowawezesha vijana kujitegemea.

Kuhusu program ya Mpira Fursa inayotolewa na vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC's) kuaagiza maafisa wa TAMISEMI  wanaoshughulia Michezo kuitumia KTO katika mahitaji ya mipira mashuleni kwa kuwa mipira hiyo hutengenezwa katika vyuo vya maendeleo ya wananchi (FDC's,) nchini.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu kwa Watu Wazima lililofanyika Kibaha Mkoani Pwani na kupongeza jitihada za wadau wakiwemo KTO kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha sekta ya Elimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akisaini kitabu cha wageni pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa KTO wakiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maggid Mjengwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde (kulia,) akizungumza na wafanyakazi wa KTO wakiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maggid Mjengwa mara baada ya kuwatembelea na kuona shughuli wanazozifanya.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa (kushoto,) akimkabidhi nakala zinazoelekeza majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo (kulia,) mara baada ya kutembelea na kujionea shughuli zinazofanywa na KTO.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...