Na Mwandishi wetu 

Salim Sharrif  aliibuka mshindi wa jumla wa NCBA Golf Series uliofanyika katika Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana Jumamosi baada ya kufikisha pointi 76 na kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 100.

"Ninajisikia furaha kuwa mshindi wa michuano hii ya   kwanza kufanyika nchini Tanzania,”

"Asante kwa waandaaji, wachezaji wenzangu wa gofu na familia yangu kwa kuniunga mkono," alisema Sharrif.

Alitunukiwa zawadi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na safari iliyofadhiliwa kikamilifu kwenda Nairobi, Kenya ambako atashiriki fainali ya NCBA kwa nchi za Afrika ya Mashariki zitakaofanyika Desemba mwaka huu ambapo wachezaji wengine wa gofu kutoka eneo la ukanda wa Afrika Mashariki pia watachuana kuwania tuzo za kikanda.

Katika kitengo cha jumla cha wanawake, Ayne Magombe alinyakua nafasi ya kwanza kwa alama 81 na kujishindia zawadi kama hizo pamoja na safari ya kwenda Nairobi na vocha ya zawadi ya mafuta yenye thamani ya Tsh500,000.

Pia kulikuwa na washindi wengine kutoka makundi tofauti, akiwemo Amandeep Dhani, ambaye aliibuka mshindi wa Division A wanaume (0-9 handicap) baada ya kupata alama 69 na kujishindia mfuko na mtungi wa Gesi.

Fahmy Mbarak alishinda Divisheni C (wanaume) baada ya kupata pointi 74 huku kwa upande wa Ladies Division Silver ushindi ukienda kwa Marryane Mugo aliyepata pointi 77 na Catherine Mabula aliyefunga pointi 74.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Bakari Machumu, Claver Serumanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania alisema kuwa taasisi yake ya kibenki ambayo pia ipo katika nchi za Afrika ya Mashariki  imekuwa ikiandaa mashindano ya Gofu ya NCBA kwa mwaka wa nne nchini Kenya na Uganda ikiwa kwa mara ya pili na safari hii imeamua kutambulisha mashindano hayo nchini Tanzania ambapo washindi watatu wataungana na washindi wengine katika fainali nchini Kenya.

"Tunafuraha kuwa wenyeji wa michuano ya NCBA kwa mara ya kwanza hapa Tanzania,"

"Tukio hili limekuwa la mafanikio makubwa nchini Kenya na linafanyika kwa mwaka wa pili nchini Uganda,"

"Tunataka kulifanya tukio kuu la gofu katika Afrika Mashariki ili kukuza mchezo kama jukumu letu la kijamii,"

Lengo ni kuona wachezaji wa gofu kutoka nchi za Afrika Mashariki wakicheza katika michuano mikubwa kama vile PGA na michuano mengine makubwa ya gofu barani Ulaya katika miaka kadhaa ijayo.

Gift Shoko, afisa wa NCBA kutoka eneo la ukanda wa Afrika Mashariki alisema kuwa wanafuraha kujenga urafiki na Chama cha Gofu Tanzania kwa ajili ya kukuza mchezo huo.

"Tunatoa zawadi nyingi ili kuhimiza watu kujitokeza zaidi na kufanya gofu kama mchezo wa kijamii kwa kila mtu," alisema.

"Kwa hivyo tungependa kuona mfululizo zaidi wa gofu wa michuano ya NCBA ikifanyika katika viwanja mbalimbali vya gofu na tuko tayari kutoa msaada wetu kuona hilo likifanyika," alisema katika hafla ya kutoa zawadi.

Alisema mchezo wa gofu ni mchezo unaokuwa kwa kasi nchini Tanzania na unaweza kupanda hadi kiwango cha juu katika siku za usoni.

Mgeni rasmi, Machumu, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communication aliipongeza NCBA kwa kufanikisha michuano hii, huku akitoa wito kwa watu wengi zaidi kujitokeza kucheza na kuunga mkono mchezo huo mzuri.

“Mimi mwenyewe kuna watu walijaribu kunishawishi kuucheza mchezo huu hapo awali , lakini kiukweli walishindwa,”

”Hata hivyo, kuna rafiki yangu mwingine alinishawishi na hatimaye nikajikuta nacheza na kuupenda mchezo huu,”, amesema Machumu.

 "Baadaye niligundua kuwa ni mchezo mzuri na ndio maana nilikuwa sehemu ya washiriki wa michuano hii,” amesema.

 Salim Sharrif  aliibuka mshindi wa jumla wa NCBA Golf Series uliofanyika katika Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana baada ya kufikisha pointi 76 na kuwashinda wash HBiriki wengine zaidi ya 100.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...