Na Janeth Raphael - Michuzitv Dodoma

Jamii yatakiwa kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Ili kufanikisha Kampeni ya "TOKOMEZA RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA, SHULENI NA VYUONI" ili kujenga Tanzania isiyokuwa na Rushwa wala Madawa ya Kulevya.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)CP Salum Hamduni Leo Oktoba 04,2023 wakati wa uzinduzi huo uliofanywa pamoja na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA)CG Aretas J.Lyimo tukio lililofanyika Jijini Dodoma.

CP Hamduni amesema matarajio yao kampeni hiyo ikitekelezwa kwa ushirikiano na wadau wote nchini ikiwemo waandishi wa habari na wadau wote hususani katika ngazi ya elimu itachangia kuongeza uelewa kwa wanafunzi,vijana na jamii kwa ujumla kuhusu ukubwa wa tatizo la Rushwa na madhira ya madawa ya kulevya.

"Tunasema Madhira ya Dawa za kulevya kwa Sababu Vitendo Vya Rushwa na Biashara Pamoja na Matumizi ya Dawa za kulevya zina madhara makubwa Kiuchumi,kijamii na kisiasa.

"Vitendo hivi vinarudisha nyuma nguvu kazi ya Taifa kwa kusababisha ulemavu,Vifo,kuwa na walaigbu wengi wa dawa za kulevya, gharama kwa serikali katika kuwahudumia pamoja na kupoteza mapato ya Serikali" amesema CP Hamduni.

Kwa Upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA)CG Aretas J.Lyimo amesema lengo kuu la Kampeni hiyo ni kuelimisha Umma kuhusu tatizo la Dawa za kulevya na mahusiano ya ushiriki na kukabiliana na matatizo

hayo Ikiwemo rushwa pamoja na Dawa za kulevya.

"Matarajio ya Kampeni hii Kuwa yatawajengea Uwezo wanafunzi, Wanachama wa klabu za wapinga rushwa na wananchi Kwa Ujumla juu ya Uelewa Wa Tatizo la Rushwa na uhusiano wake na dawa za kulevya.

"Hapa tutapata uhusiano Wa Rushwa na Madawa ya Kulevya,hivyo wanafunzi wale tunaowafundisha Vyuoni watakuwa na Huo uelewa Wa Rushwa na madhara yake na pia hivyo hivyo Kwa madawa ya kulevya hapo tutajenga Taifa Bora" amesema Kamishna Jenerali huyo.

Aidha, CG Lyimo amesema kupitia Taasisi hizo Mbili (TAKUKURU na DCEA) wanakwenda kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi na pia wanajenga taifa la watu Wenye Uadilifu.

Kampeni hiyo inalenga kutokomeza rushwa na madawa ya kulevya kupitia klabu za wapinga rushwa na madawa ya kulevya mashuleni na vyuoni kwa nchi nzima. Pia itawafikia vijana ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa elimu


Pichani kulia ni CP. Salum Rashid Hamduni, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na kulia kwake ni Kamishna Jenerali Aretas James Lyimo, Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya (DCEA) wakati wa uzinduzi huo Oktoba 4, 2023 jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...