Na.Khadija Seif, Michuziblog
WASANII Waaswa kujitokeza kwa wingi katika matamasha yanayo waunganisha wasanii kutoka mataifa mbalimbali ili kubadilishana utamaduni na kuongeza wigo wa kazi zao kujitangaza.

Akizungumza na Michuziblog Mkurugenzi wa Taasisi ya Nafasi arts space wakati wa uzinduzi wa Tamasha la ' Wikiendi lives' Lilian hipoliyte amesema Tamasha hilo limerudi kwa kishindo na kuwapa nafasi jukwaa hilo kwa wasanii wakitanzania kuboresha sanaa zao ,kujitanua na kupata kukutana na mashabiki zao na wengi wapya.

"Tamasha la wikiendi linaratibiwa na Nafasi arts space kwa kushirikiana kwa karibu na Ubalozi wa Norway pamoja na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania ambapo tamasha hili mara ya mwisho lilifanyika mwaka 2014 kutokana na sababu mbalimbali hivyo mwaka 2023 tumelizindua tena ."

Hata hivyo amesema kuwa wasanii wa Kitanzania wameshiriki katika tamasha hilo kwa Sanaa za ngoma na Sanaa za uoni pamoja na uchoraji kwa watoto huku Msanii grace Matata akisherehesha Uzinduzi huo.

"Tamasha hili limelenga kuwapa fursa wasanii mbalimbali kuonesha kazi zao na ndio maana tunajumuisha sanaa zote hata watu wa sarakasi kwa sababu tuna amini kupitia tamasha hili linawapa fursa wale wasanii ambao hawatambuliki kutambulika kwa urahisi na kuongeza mashabiki kutoka mataifa mengi."

Aidha ameeleza faida ya kuwepo kwa tamasha sio tu wasanii kupata kutumbuiza bali wasanii wa Sanaa za uchoraji na ushonaji wanapata nafasi ya kuuza kazi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...