Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Octoba 4,2023 amepokea magari 10 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya Shilingi Bil. 1.1 kutoka Serikali ya India.
Waziri Ummy wakati akipokea magari hayo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam ameishukuru Serikali ya India kupitia kwa Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Pradhan kwa msaada huo ambao unaendelea kuonesha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
“Serikali ya India imekua na ushirikiano Mkubwa na Serikali ya Tanzania ikiwemo katika Sekta ya Afya, hivyo nitumie fursa hii kuwashuku sana kwa msaada wa magari haya ambayo hata kwenda kusaidia kurahisisha huduma kwa Watanzania”. Amesema Waziri Ummy
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...