Na. WAF - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeitaka jamii kuwekeza zaidi katika afya ya akili kipindi hiki ili kusaidia kukomesha ukiukwaji  wa haki za binadamu ambazo watu wenye changamoto za afya ya akili wanaendelea kukumbana nazo siku hadi siku.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito huo leo Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani yaliyofanyika Dodoma kitaifa  ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu 2023 ni 'Afya ya akili ni haki kwa binadamu wote’.

Ameeleza kuwa Tatizo la Afya ya Akili ni tatizo la kila mtu ili kumaliza tatizo hilo lazima kushikamana kwa pamoja na siyo kuwatenga na kuwanyanyapaa watu wenye changamoto hiyo.

“Lengo kuu la maadhimisho haya ni kujenga na kuongeza ufahamu wa wananchi juu ya madhara  yatokanayo na matumizi ya pombe yaliyokithiri pamoja na  kutafakari hali halisi na mwelekeo wa udhibiti wa matumizi haya Kitaifa na Kimataifa, kama tujuavyo matumizi ya pombe yanaleta changamoto kubwa ya uraibu na magonjwa ya akili”. Amebainisha Dkt. Mollel.

Kwa upande wake Bi. Monica Isaya ambae alishawahi kupata changamoto ya Afya ya Akili ametoa rai kwa wananchi kuacha  kutumia dawa za kulevya, kutokuwa na msongo wa mawazo pamoja na kujua kufanya jambo gani kwa wakati upi.

“Changamoto hii ya Afya ya Akili inatupata sana sisi wakina mama kwa sababu nyingi ikiwemo kuachwa, kupokonywa mali na watoto pamoja na kujiingiza kwenye mikopo”. Amesema Bi. Monica.


Pia, amesema kuanguka barabarani ambapo unaweza kugongwa na gari na kupelekea ulemavu, kuwa mkali kupitiliza, kutembea bila nguo, kuuwa, kuombaomba, hayo yote ni madhara ya Arya ya Akili.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...