Injinia Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Onesphori Kamukuru akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo 11Novemba 2023 Mkoani Manyara juu ya fursa ambazo vijana wanaweza kuchangamkia ili kujikwamua kiuchumi
Afisa Elimu Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Martha Ngalowera akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Manyara katika maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa .
Na.Vero Ignatus,Manyara
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo athari za mabadiliko hayo zimeonekana katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini ikiwemo sekta kilimo, mifugo maji nishati, maliasili miundombinu na usafirishaji.
Aidha athari hizo ni pamoja na matukio ya ukame, mafiriko, maporomoko ya udongo ongezeko la joto kuibuka,milipuko wa magonjwa ya mazao, mifugo na binadamu pamoja na uwepo wa viumbe vamizi jamii maskani haswa vijijini huathiriwa zaidi na mabadiliko haya.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho wa wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Manyara Mhandisi Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Onesphori Kamukuru amesema lengo la kushiriki ni kuendelea kutoa elimu juu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira pamoja na fursa mbalimbali kwa Vijana ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kamukuru amesema katika maonyesho hayo watakuwa na mada juu ya nafasi ya vijana katika Uhifadhi wa Mazingira pamoja na kuongeza kipato, uhifadi wa taka, kilimo hifadhi , uhifadhi wa taka na urejeshwaji wa wa taka utakaowapatia kipato na kuhifadhi mazingira.
"Kuna miradi ambayo vijana wanaweza kufuatilia jama wa taka ngumu ,urejeshwaji wa taka viwandani, zitakazowasaidia kukuza uchumi wao, vijana waanae maandiko wayalete tuyapitie sisi tutawasaidia kutafuta wafadhili mfano biashara ya carbon kwakutunza misitu ili waweze kunufauka"
Kamukuru amewasihi vijana kabla hawajaingia kwenye shughuli za mazingira ni vyema wapate miongozo na kanuni za utunzaji wa mazingira kama vile ambavyo mkakati wa utekelezaji wa sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 kwa kipindi cha 2022- 2023 ambapo mkakati huo umebainisha mikakati ya utekelezaji kwaajili ya kukabikiana na changamoto na masuala mtambuka katika usimamizi wa mazingira
Kwa upande wake Afisa Elimu Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amewataka vijana kuchangamkia mradi wa biashara ya Caboni kwa kutunza mazingira kwa kuotesha miti mbalimbali kwani mbali na kuotesha pia itawapatia kipato kwaajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku
"Ozoni inapoharibika kunakuwa na mabadiliko ya tabianchi, kama mnavyoona kwasasa joto ni kali, hivyo vijana mkiweza kuotesha miti katika maeneo mbalimbali mtaiuza mtapata kipato pia mtatinza mazingira.
Ngalowera amewataka wanawake kwa vile wao ndiyo watumiaji wazuri wa mazingira wanayo fursa kuanzisha vitalu vya miti pamoja na kuzalisha taka za vyakula kama mbolea bora isiyokuwa na madhara na kunyunyunyiza kwenye mbogamboga na wakapata kukuza uchumi
Ngalowera amesema kuwa wapo kwaajili ya kutoa elimu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa nchi mbili ulioasisiswa 12januari 1964 kwani vijana wengi walikuwa hawafahamu muundo, hali pamoja na Misingi ya Muungano.
Ambapo ametaka Vijana watambue kuwa Misingi ya Muungano Mazingira wezeshi , unatokana na ukaribu udugu wa damu , kufanana kwa tamaduni, lugha ya kiswahili na kushahabiana kwa matukio ya kihistoria katika utumwa, ukoloni na harakati za uhuru, kuishi na matarajio ya waasisi wa muungano, misimamo, falsafa, dira, kauli namatendo ya viongozi.
Ilikukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na jamii kwa ujumla kuhimili athari za mabadiliko kwa shughuki mbadala za kujiongezea kipato , upatikanaji wa maji, matumizi ya majiko bunifu hifadhi ya misitu na upandaji wa miti na kuongoa maeneo yaliyoharibika na nyanda za malisho, pia upatikanaji wa taarifa kwa umma kuhusu mbinu bora za kukabikianana athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mifumo ya ikolojia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...