Na Muhidin Amri, Chunya


WAKALA wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa),imefanikisha kumaliza kero ya muda mrefu ya huduma ya maji 
safi na salama kwa wakazi  wa kijiji cha Sangapi Halmashauri ya wilaya Chunya mkoani Mbeya baada ya kujenga  wa mradi mkubwa wa maji.

Kaimu meneja wa Ruwasa 
wilayani Chunya David Nyambulapi alisema,mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya Sh.milioni 507 kwa kumtumia mkandarasi chini ya usimamizi wa ofisi ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Chunya na umeanza kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 6,779 wa kijiji hicho.

Alitaja kazi  zilizofanyika 
ni kuchimba kisima chenye uwezo wa kuzalisha lita 12,000 kwa saa,uvutaji wa umeme umbali wa kilomita 1.2,ujenzi wa vituo sita vya kuchotea maji,uchimbaji wa mitaro na kulaza bomba urefu wa kilomita 23.

Kwa mujibu wa Nyambulapi,kazi 
nyingine zilizotekelezwa ni kujenga nyumba ya mashine(pump house) kujenga uzio eneo la tenki na kujenga tenki  lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 150,000 ambalo linatoshelesha kuhudumia wakazi wa kijiji hicho chenye shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo uchimbaji wa dhahabu.

Aidha alisema,katika 
uendeshaji wa mradi huo changamoto kubwa ni kukatika mara kwa mara  kwa umeme ambao umeathiri mpango wa  Ruwasa kufikisha  huduma bora ya maji kwa wananchi.

Alisema,wanatumia mashine 
kusukuma maji kutoka kwenye chanzo hadi kwenye vituo vya kuchotea maji,hivyo kupsababisha upungufu wa maji kwa baadhi ya maeneo.

Katika hatua nyingine 
Nyambulapi alisema,serikali imetoa kiasi cha Sh.milioni 100 kwa ajili ya kupeleka  huduma ya maji safi na salama kwa  baadhi ya maeneo/vitongoji ambavyo bado haijafikiwa na huduma hiyo.


Kwa upande wake Diwani wa 
kata ya  Sangambi Junjulu  Mhewa,ameishukuru serikali kuipatia fedha Ruwasa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ambao umesaidia kumaliza changamoto ya maji katika kijiji hicho na maeneo mengine  wilayani Chunya.


Alisema,kabla ya mradi huo 
wananchi wa kijiji hicho walilazimika kutembea umbali  wa masaa mawili hadi matatu kwenda kutafuta kwenye makalongo na visima vilivyochimbwa na wananchi wenyewe.


Mwenyekiti wa serikali ya 
kijiji cha Sangambi Lusekelo Lwesya,ameiomba serikali kufikisha huduma ya maji kwenye vitongoji  vikiwemo vya Izumbi ambavyo havijafikiwa na mtandao wa maji ya bomba.


Naye mwenyekiti wa mradi wa 
maji Sangambi Flora Ndukwa  alisema,mgao wa umeme umechangia kurudisha nyuma jitihada za kutoa huduma ya maji, kwani tenki linalotumika kusambaza maji kwenda kwa wananchi halipokei maji ya kutosha kutoka kwenye chanzo.


Ameiomba serikali kupitia 
wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa),kutafuta ufumbuzi wa  kero hiyo ambayo imeathiri upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.


Mkazi wa kijiji cha hicho 
Maneno Ngaponda,ameshauri wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanajaza maji ya kutosha kwenye tenki pindi umeme unapowaka ili kuepuka upungufu wa maji. 

Mwenyekiti wa mradi wa maji wa Sangambi wilaya ya Chunya mkoani  Mbeya Flora Ndukwa kushoto akimtwishwa ndoo ya maji mkazi wa kijiji hicho ambaye hakutaka kutaja jina lake wakati ukaguzi wa miundombinu ya mradi huo.

Muonekano wa nyumba ya  mashine ya kuvutia maji(Pump House)iliyojengwa kupitia mradi wa maji Sangambi Halmashauri ya wilaya Chunya mkoani Mbeya kwa gharama ya zaidi ya Sh.milioni 5.
Tenki  lenye uwezo wa kuhifadhi lita 150,000 za maji ambalo linahudumia zaidi ya wakazi 6,779 wa kijiji cha Sangambi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...