Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bweni ya Wavulana Oswe wametakiwa kuachana na matumizi ya simu za mkononi ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuepukana na wimbi la mmomonyoko wa maadili katika makuzi yao na kupelekea kupoteza malengo kwenye masomo yao.

Akizungumza na wanafunzi hao Oktoba 17, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya, alisema kwa sasa jamii imekumbwa na changamoto nyingi hasa kwenye suala la malezi ambalo limepelekea watoto wengi kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa.

Aidha, kamanda Mallya aliendelea kuwasihi wanafunzi hao kuchagua aina ya marafiki ambao watakuwa kimbilio kwao  na msaada katika makuzi yao.

Kamanda Mallya mbali na hayo lakini hakusita kutoa wito kwa wanafunzi pamoja na walimu wao kiendelea kuwajenga wanafunzi hao na kuwafundisha masuala mbalimbali ikiwemo athari za matumizi ya dawa za kulevya, kujihusisha kimapenzi wangali katika umri mdogo sambamba na kutambua haki na wajibu wao.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...