Na Jane Edward, Arusha

Mkurugenzi wa Taasisi ya tiba asili na tiba mbadala ya Kazoba International Products amewataka wananchi kuacha kula vyakula visivyozingatia vina saba ili kujiepusha na magonjwa yasioambukiza

Kazoba ameyaeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake mapema hii leo ambapo amesema ulaji wa vyakula usiozingatia lishe bora ni chanzo cha magonjwa yasio ya lazima na yasio ambukiza

Aidha amefafanua kuwa kwa sasa kumekuwa na changamoto ya ulaji wa vyakula visivyo vya asili na hivyo kusababisha ongezeko la uzito uliopitiliza na hivyo kusababisha mwili kupata magonjwa

"Ulaji wa vyakula usiozingatia vina saba vinasababisha mwili kupata magonjwa ya mfumo wa mwili kutokana na mkinzano unaojitokeza wakati wa umengenyaji wa vyakula husika".Alifafanua Kazoba

Aidha Kazoba ambae ni muuzaji wa dawa za tiba asili akawataka wananchi kwenda katika maduka mbalimbali ya Kazoba yaliyoko nchi nzima yanayotoa dawa zinazopambana na magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa vyakula usiozingatia vina saba

Hata hivyo aliyataja magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula ambavyo havijazingatia vina saba kuwa ni pamona na vidonda vya tumbo,moyo,presha,nguvu za kiume,kisukari na mengineyo

Amesema pia ulaji wa vyakula vinavyozingatia vina saba huchangia ongezeko la madini ya Zinc Potasium na Calcium ambayo husaidia kutopata magonjwa mbalimbali hususan kwa kina baba kupoteza uwezo wa kushiriki tendo la ndoa

Amevitaja vyakula ambavyo huongeza madini mwilini kuwa ni pamoja kunde,mbogamboga na maharage huku akiwataka wananchi kupata huduma za kiafya mapema pindi wanapokuwa na changamoto za kiafya

Mkurugenzi wa Kazoba akitoa elimu kuhusiana na tiba mbadala jijini Arusha.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...