Na Jane Edward, Arusha
Washiriki zaidi ya 1300 wanatarajiwa kuhudhuria Kikao cha sabini na saba cha kawaida cha kamisheni ya Afrika ya haki za binadamu na watu ambacho kinatarajia kufanyika kwa siku ishirini jijini Arusha ambapo maswala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo uzinduzi wa nyaraka mbalimbali za kamisheni ya haki za binadamu Afrika .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Balozi Dkt Pindi Chana amesema Kikao hicho kimelenga kutoa elimu juu ya haki za binadamu ikiwemo kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.
Chana amesema mpaka sasa waliojiandikisha ni washiriki Mia saba kati ya 1300 ambao wanatarajiwa kufika katika Mkutano huo ambapo Tanzania ndiyo wenyeji wa Mkutano huo.
Amesema kimsingi Mkutano huo una endelea kujenga uhusiano wa kimataifa katika wizara mbalimbali hapa nchini ikiwemo wizara ya Utalii pamoja na wizara zingine.
"Kikao hiki kitawezesha pia sekta ya utalii kupata watalii watakao kwenda kutalii katika mbuga za wanyama na kutembelea vivutio mbalimbali"Alisema Balozi Chana
Aidha ametoa wito kwa wanachi wa Arusha kuhakikisha wanaendelea kuwa wakarimu na kuzungumzia uzuri wa nchi yao kwa wageni hao ili kuwezesha wageni kuondoka salama huku kukiwa na sifa ya ukarimu.
Akizungumzia maandalizi ya Mkutano huo Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano( AICC) Ephraim Mafuru amesema Mkutano huo umekuwa ni wa manufaa makubwa kuja jijini Arusha na wameandaa watoa huduma ngazi ya Kimataifa watakao wahudumia wageni hao.
Katika kuonyesha faida za uwepo wa Mkutano huo amesema Tanzania itaingiza kiasi cha shilingi dola za marekani zaidi ya Milioni saba laki tano na elfu sitini ambapo kwa fedha za Kitanzania ni zaidi ya Bilioni 18.9 katika uchumi wa Kitaifa.
"Tumeandaa huduma zote za kimikutano pamoja na watoa huduma na mpaka sasa hali ya maandalizi ni nzuri na inavutia kwaajili ya wageni hao"Alisema Mafuru
Hata hivyo Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar Dr Hussein Ally Mwinyi Rais wa Mapinduzi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) Ephraim Mafuru akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...