Katika jitihada za  kuinua uchumi wa bluu nchini, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega amekabidhi boti 8 za uvivu kwa vikundi vya akina mama,vijana na watu binafsi  zitakazo saidia kuinua uchumi wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi boti hizo wakati wa ziara yake ya  kukagua shughuli za maendeleo katika kata ya Kisiju, wilayani Mkuranga mkoani pwani Oktoba 9, 2023,  waziri ulega ametoa rai kwa wanufaika wa boti hizo kuzitunza na kuzitumia vyema ili waweze kuboresha shughuli zao.

Aidha ameongeza kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa ubunifu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuinua maisha ya wananchi kwa vitendo.

Boti hizo 8 alizozigawa Waziri Ulega ni miongoni mwa boti 168 zenye thamani ya bilion 11.6 ambazo zimetolewa na Rais, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan nchi nzima.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...