WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyeshe ya Kuku na ndege wafugwao Tanzania (Tanzania Poultry Show) ambayo yatafanyika tarehe 13 hadi 14 Oktoba 2023, Mlimani City Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 05,2023 Jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Maonesho hayo Sufian Zuberi amesema Maonesho yanafanyika kwa msimu wa nane ambapo yatashirikisha wadau mbalimbali wa Mnyororo wa thamani kwa Kuku na ndege wafugwao.
"Maonesho haya tuna wadau mbalimbali ambapo tunawajumuisha wakiwemo wazalishaji wa vyakula vya mifugo,watotoleshaji wa vifaranga,wauzaji wa virutubisho na vichanganyio mbalimbali pamoja na wataalam wa tiba ya chanjo kwa mifugo."
Pia amesema katika Maonesho hayo kutatolewa semina na Mafunzo kutoka kwa wataalam mbalimbali namna ipi bora ya Ufugaji wa Kuku.
Aidha amebainisha Malengo ya Maonesho hayo ni kuwapa mafunzo ili wafugaji waweze kuendana na kasi ya ufugaji wenye tija ,Kuhakikisha mazao na nyama inayotokana na Mifugo hiyo inakuwa salama kwa matumizi na kujali Afya ya mlaji.
Hata hivyo ameeleza kuwa soko la Ufugaji wa Kuku linakuwa kwa Kasi kutokana na mahitaji ya walaji wengi hivyo wafugaji wapya wanaongezeka ni muhimu elimu ya Ufugaji ikitolewa.
"Kutokana na idadi kubwa ya watu hata ongezeko la walaji wa kuku inakuwa kubwa sababu kubwa na kielelezo tosha cha walaji wa kuku ni Uwepo wa Protini nyingi kwenye Kuku na mazao yake."
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya uzalishaji wa Chakula cha Mifugo nchini Vicent Nyingi amesema ni Fursa nzuri kwao kama wadhamo wa Maonesho hayo ya kutoa elimu kwa Wazalishaji wadogo wadogo na kukuza tasnia ya Kuku nchini.
''Sisi kama wadhamini tumeona ni fursa nzuri ya kuwepo kwenye maonesho haya kwa wafugaji ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za ufugaji wa Kuku na mayai ."
Nyingi amewataka Watanzania kufika kwa wingi kwa ajili ya kujifunza na kujionea fursa mbalimbali katika tasnia hiyo na kujadili mitindo ya namna ya kuboresha Ufugaji sahihi wa Kuku na Afya ya mifugo hiyo .
"Tutajadili maswala ya Afya ya utumbo kwenye Kuku hivyo ni maswala ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele zaidi ili kumhakikisha mlaji usalama wa Afya yake kupitia Protini bora anayoipata kwenye Kuku na mayai." Mratibu wa Maonesho ya Kuku na ndege wafugwao nchini (TANZANIA POULTRY SHOW) Sufian zuberi akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 10,2023 Jijini Dar es Salaam mara ya kutangaza rasmi ujio wa Maonesho ya Kuku na ndege wafugwao nchini (TANZANIA POULTRY SHOW) yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 13 hadi Oktoba 14,2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Wizara wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...