ZAIDI ya watu 1,000 wamehudhuria kwenye kambi maalum ya afya iliyoendeshwa na klabu za Rotary za Dar es Salaam na Bahari zikishirikiana na wadau mbaimbali katika viwanja vya shule ya msingi Bunju A jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Kambi hiyo ilijumuisha madaktari takribani 100 - wakiwemo madaktari wa kawaida 50 na wataalamu wengine 50 wa meno, macho, ngozi, watoto, magonjwa yasiyoambukiza na huduma nyingine za afya ambapo walitoa huduma za upimaji, ushauri na matibabu bure kwa wananchi waliofika katika kambi hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi hilo, wananchi waliopatiwa huduma hizo wameupongeza mpango huo wa Rotary wa kuandaa kambi hiyo na kutoa huduma hizo bure kwa wananchi wote.

“Hii ni Faraja kubwa sana kwetu hususan sisi tusio na uwezo wa kugharimia matibabu.

Tunaomba serikali na wadau wengine waendelee kuiunga mkono Rotary ili iweze kufanya kambi hizi ziwe za mara kwa mara. Hii itatusaidia sana” alisema Mariam Mbaruku mkazi wa Mapinga Bagamoyo.

Marais wa klabu za Rotary za Dar es Salaam na Bahari Nikki Aggarwal na Jumana Zavery wamesema kuwa zoezi hili ni muendelezo wa kambi za afya zinazofanywa na klabu za Rotary wakishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wizara ya Afya na mashirika na makampuni mbalimbali katika kutekeleza moja ya azma za Rotary ya kutoa huduma za Afya ya jamii bila gharama.

Rotary hufanya jukumu hili kama sehemu ya msingi wake mkuu wa kusaidia jamii zenye uhitaji.

Kambi hiyo imefanywa kwa ushirikiano na Vilabu vya vijana wa Rotary vya Kairuki, Muhimbili, KIUT, Alpha, na Kwanza na kufadhiliwa na Bill & Melinda Gates Foundation, Pepsi, SGA Security, Agha Khan Health Service Tanzania, Minet Insurance Brokers, G1 Logistics Ltd, Colgate Palmolive, Chemi & Cotex Industries, Planet Pharmaceuticals Limited, na Management and Development for Health (MDH)."

 

Watoto ni miongoni mwa wakazi  wa Bunju na maeneo ya jirani waliohudhuria kambi maalum ya kutoa huduma  za afya iliyoandaliwa na klabu za Rotary za Dar es Salaam na Bahari katika shule ya msingi Bunju A mwishoni mwa wiki. Zaidi ya wananchi 1,000. walipatia huduma za afya ikiwemo vipimo, matibabu na ushauri bure wakati wa zoezi hilo.
 

Wakazi  wa Bunju na maeneo ya jirani wakiwa wanasubiri huduma za afya wakati wa kambi maalum ya afya iliyoandaliwa na klabu za Rotary za Dar es Salaam na Bahari katika shule ya msingi Bunju A mwishoni mwa wiki. Zaidi ya wananchi 1,000. walipatia huduma za afya ikiwemo vipimo, matibabu na ushauri bure wakati wa zoezi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...