KAMPUNI ya Startimes limited wameamua Kumaliza mwaka 2024 kwa maudhui ya Kiburudani wazindua rasmi Msimu wa tano wa Reality show "Hello Mr.Right."

Akizungumza na Wanahabari Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na wateja wa Startimes na tayari wamepokea ofa ya Kampeni ya "Lipa tukubusti" imewalazimu kuzindua Msimu mpya wa reality show (HELLO MR.RIGHT) msimu wa tano inayolenga zaidi vijana katika kutafuta wenzao wao.

Hata hivyo Malisa ameongeza kuwa Msimu mpya wa Kipindi hicho kitakuwa na ingizo jipya la Mtangazaji ambae mpaka sasa hajatambulishwa hivyo kibarua kimeachwa kwa watazamaji wa Startimes kupitia kurasa z instagram kubashili Mtangazaji huyo atakuwa nani.

"Kila msimu tumekuwa wa kitofauti zaidi kuanzia mandhari ya eneo husika hivyo tumeamua kwa upande wa watangazaji tuongeze nguvu ya Mwanadada ambae anafahamika zaidi lakini alikuwa nje kidogo ya media lakini Hello Mr.right inaenda kumrudisha ambapo atakwenda kusaidiana na Mc garab pamoja na Lulu diva katika steji.

Sanjari na hilo amesema kipindi hicho kinalenga zaidi kuwapa fursa vijana kutafuta wenza kitakuwa kikiruka chaneli ya st bongo ambapo Vijana hao watapata fursa ya kupatiwa elimu ya Afya .

''Kisimbuzi chetu cha Antena unaweza kukipata kwa bei ya Sh 25000 kisimbuzi peke yake huku ukilipia kifurushi cha Mambo sh 17000 kwa mwezi na bado tutakupandisha na Kisimbuzi Full set inapatikana kwa sh 41000 huku ukilipia kifurushi cha Mambo sh 17000 nasi tutakupandisha hadi Uhuru kwa mwezi mzima Bure." Ameongeza Malisa

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Kampuni Quantum infinity Magreth Lawrence amewakaribisha Makampuni na taasisi mbalimbali kudhamini show hiyo kwani King'amuzi cha Startimes kinaongozwa kutazamwa nchini Tanzania kwa sasa.

"Wote tunajua Hello Mr.Right ni show ya Vijana 100% hivyo tumejipanga zaidi kukutanisha Vijana kutoka sehemu mbalimbali kupitia jukwaa hili kujifunza vingi na kupata fursa mbalimbali hivyo ni wakati wa taasisi na Makampuni kutangaza biashara zao kupitia kipindi hicho. "


Hata hivyo Mtangazaji wa Kipindi hicho Mc garaB amesema kumekuwa na Kauli mbiu Mmbalimbali tangu kuanza kwa Shindano hilo huku akitaja msemo mwaka huu utatumika "Kaa kwa kutulia".


Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 28,20,2023  wakati akizindua Msimu wa tano wa Reality show (HELLO MR.RIGHT) Jijini Dar es Salaam

 

Mc Garab akieleza namna Msimu wa tano wa Kipindi cha Hello Mr.Right. kilivoboreshwa kuanzia mandhari, kauli mbiu pamoja na ingizo jipya la Mtangazaji atakaesaidiana nae kuendesha Kipindi hicho .
 

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Kampuni Quantum infinity Magreth Lawrence akizungumza machache na Wanahabari mara baada ya kuzinduliwa kwa Msimu wa tano wa Reality show ya Hello Mr.Right itakayoanza rasmi Disemba 02,2023

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...