Mkutano huo umeanza katika Ngazi ya Wataalam wanakutana jijini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2023 na utafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 21 Novemba 2023, na kufuatiwa na Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023.
Mkutano wa ngazi ya Wataalam unapitia na kujadili masuala mbalimbali kuhusu Mtangamano wa Afrika Mashariki ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri kwa mapendekezo.
Masuala yanayojadiliwa katika Mkutano huo wa wataalamu ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 - 24 Novemba, 2023; Taarifa ya utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya kuhusu; Majadiliano ya Jamhuri ya Somalia kujiunga na Jumuiya; Hatua iliyofikiwa katika kutafuta Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo ya mchakato wa kijeshi na uongezaji muda wa mkataba wa SOFA; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya ya Afrika; majadiliano ya Katiba kuhusu Katiba ya Fungamano la kisiasa Afrika Mashariki; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na; Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya Uandishi wa insha kwa wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo unahudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Uganda, Rwanda, na Sudan Kusini.
Baada ya kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 23 Novemba utafanyika Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira na kufuatiwa na Mkutano wa kawaida wa 23 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya uliopangwa kufanyika jijini Arusha tarehe 24 Novemba, 2023.
Ujumbe
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki katika Mkutano wa
kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki
ngazi ya wataalamu unaofanyika jijini Arusha tarehe 18 -20 Novemba 2023
Wajumbe
wa meza kuu wakiongoza Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri
la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Wataalamu unaoendelea
jijini Arusha, Mkutano huo unafanyika tarehe 18 -20- Novemba 2023
jijini Arusha utafuatiwa na kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu
kitakachofanyika tarehe 21 Novemba na baadaye kufanyika mkutano wa
Baraza la Mawaziri tarehe 22 Novemba, 2023.
Wajumbe
kutoka katika Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Rwanda na Jamhuri ya Kenya
wanaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la
Jumuiya ya Afrika Mashariki uli
oanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu
Wajumbe
kutoka Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
wanaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la
Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini
Arusha katika ngazi ya Wataalamu
Wajumbe
wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya
ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha
katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao
Wajumbe
wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya
ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha
katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao
Wajumbe
wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya
ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha
katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao
Home
HABARI
Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza jijini Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...