*Yaipongeza KTO, kuendelea kufadhili miradi ya michezo

SHIRIKISHO La Mpira barani Ulaya (UEFA,) limeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali ya Karibu Tanzania Organization (KTO,) kwa jitihada zinafanywa katika kukuza soka la wanawake na wasichana katika ngazi mbalimbali za Elimu kwa kuanzia ngazi ya Elimu Msingi.

Hayo yameeelezwa Leo jijini Dar es Salaam na mtaalam wa michezo kutoka UEFA Carine Nkoue aliyetembelea shule za Uhuru, Kibugumo na Gezaulole zilizopo jijini Dar es Salaam kupitia taasisi ya UEFA Foundation For Children ambao ni mahususi kwa kuendeleza soka kwa watoto na vijana ambapo Tanzania kupitia Program ya Mpira Fursa inayotolewa na KTO kupitia Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi imekuwa mnufaika pekee wa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema, Tanzania inafanya kazi nzuri kupitia washirika wao wa KTO na amejionea namna mabinti wanavyojenga ujasiri kupitia soka la wanawake na wasichana.

"Mpira wa miguu sio kucheza pekee bali ni ajira, inajenga kujiamini kwa mabinti na kusaidia kujenga timu imara....kwa mchezo huu nilioshuhudia nina imani mabinti hawa watajenga timu imara zaidi katika level za juu....Tunategemea kuwaona katika soka la Dunia." Amesema.

Aidha amesema kuwa, UEFA itaendelea kusimamia na kushiriki katika miradi ya namna hiyo katika kuhakikisha soka hususani kwa watoto wa kike linakuwa zaidi.

Pia amewapongeza walimu wa Shule za Msingi Kibugumo, Uhuru na Gezaulole kwa kujitoa na kuhakikisha wanafunzi wanashiriki katika soka pamoja na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa Pete na kriketi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa KTO Maggid Mjengwa amesema kupitia program ya Mpira Fursa inayotolewa katika vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi imekuwa na matokeo chanya; kwa miaka minne ya utekelezaji wake umetoa wanawake wacheza soka, makocha wanawake pamoja na viongozi hali inayopelelea kukua kwa mpira wa miguu Tanzania.

Mjengwa amesema, ujio wa UEFA nchini ni kielelezo kuwa sekta ya michezo nchini ipo katika anga za kimataifa na hiyo ni kutokana na jitihada zinafanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya michezo kuanzia ngazi ya Elimu Msingi.

"Tutaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, TAMISEMI na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF,) katika kusongesha gurudumu hili mbele zaidi.......UEFA imeielewa na inaiamini Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya namna hii na sisi KTO tutaendelea kutafuta Fursa zaidi kutoka UEFA ili sekta ya michezo iendelee kukua zaidi kimataifa." Amesema.

Amesema kuwa shule za Msingi 110 ambazo zipo karibu na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC's) kote nchini zinanufaika na program ya Mpira Fursa ambayo pia imechangia katika kupunguza utoro kwa wanafunzi pamoja na kuwajengea mabinti kujiamini.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Wilaya ya Kigamboni Lucas Ouma ameishukuru UEFA kupitia mradi huo kwa watoto na kuahidi kuendelea kuhimiza programu ya michezo mashuleni kwa vitendo.

Amesema, wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO,) katika kuhakikisha wanawajenga watoto kimichezo kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Pia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Gezaulole Mariam Kinande amesema, wamekuwa wakihamasisha wanafunzi kujiunga na michezo na takribani wanafunzi wa kike wapatao 64 wanashiriki mchezo wa Mpira wa miguu.

Katika ziara hiyo Bi. Carine Nkoue ameshuhudia mechi ya kirafiki kwa timu za Wasichana wa Shule za Msingi kati ya Gezaulole ambayo iliibuka na ushindi wa mbao 2 -0 dhidi ya Kibugumo.

Mtaalam wa michezo kutoka Shirikisho la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kitengo cha UEFA Foundation For Children Taasisi maalum ya kuendeleza soka kwa watoto na vijana Carine Nkoue akiwa katika picha ya pamoja na timu ya soka ya wasichana kutoka shule ya Msingi Gezaulole  Leo jijini Dar es Salaam.
Mechi ikiendelea
Mtaalam wa michezo kutoka Shirikisho la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kitengo cha UEFA Foundation For Children Taasisi maalum ya kuendeleza soka kwa watoto na vijana Carine Nkoue akiwa katika picha ya pamoja na timu ya soka ya wasichana kutoka shule ya Msingi Kibugumo  Leo jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa michezo kutoka Shirikisho la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kitengo cha UEFA Foundation For Children Taasisi maalum ya kuendeleza soka kwa watoto na vijana Carine Nkoue akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa darasa la tatu ambao ni wanufaika wa program ya Mpira Fursa  kutoka shule ya Msingi Kibugumo  Leo jijini Dar es Salaam.
Matukio mbalimbali wakati wa ziara ya mtaalam wa michezo kutoka UEFA Bi. Carine Nkoue nchini Tanzania, Ziara hiyo imelenga kukagua utekelezaji wa program ya Mpira Fursa inayotolewa na (KTO,) mahususi kwa kukuza soka la wanawake na wasichana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...