Maadhimisho ya tatu wiki ya huduma za fedha Kitaifa yameanza rasmi leo Jijini Arusha 20/11/2023 ambapo yameamdaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha nchin, ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya Fedha wa mwaka 2020/21-2029,kipaumbele kikiwa ni kutoa elimu kwa umma katika utekelezaji wa mpango huo sambamba na kupunguza umaskini.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha Kamishna wa Idara ya uendelezaji wa Sekta ya fedha Dkt.Charles Mwamwaja juu ya maaadhimisho hayo ,alisema kuwa Tanzania ifikapo mwaka 2025 asilimia 80%watakuwa wamepata uelewa wa huduma za kifedha ikiwemo benki masoko na dhamana za mitaji huduma za bima ,huduma za mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi
Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya fedha inajitahidi kuhakikisha kuwa wa wawe wamefikiwa na huduma hizo kwa kutoa elimu ya umuhimu wa matumizi ya huduma hizo.
Alisema kuwa kutokana na utafiti wa Finscope wa mwaka 2023 nchini ni asilimia 53.8 tu ya nguvu kazi wanatumia rasmi huduma rasmi za fedha ambapo kundi kubwa la watanzania halifaidiki na huduma hizo na kusababisha kukosa fursa za kuboresha Maisha kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zingewawezesha kukuza na kuchangia pato la Taifa.
Dkt.Mwamwaja amesema kuwa malengo ya wiki hiyo ya huduma ya kifedha ni pamoja na Kujenga uelewa na weledi kwa umma katika matumizi sahihi ya huduma za kifedha ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini, Kuimarisha ufanisi wa Masoko ya Fedha kupitia elimu ,Kuongeza upatikanaji wa huduma jumuishi,, Kutoa elimu ya kumlinda mtumiaji wa huduma,Kuwezesha wananchi kusimamia vizuri rasilimali fedha,kuwezesha wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na matumizi sahihi ya huduma za kifedha katika kukuza biashara zao.
‘’Maadhimisho hayo ni pamoja na mambo mengine yanalenga kuwajengea wananchi huduma ya uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za kifedha sambamba na Kuimarika kwa utamaduni wa kujiwekea akiba, kukopa na kulipa madeni,na Kuongezeka kwa mchango wa Sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa uchumi’’.Alisema Dkt.Mwamwaja.
Dkt.Mwamwaja aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwaunganisha wananchi wajasiriyamali na wadau wengine ili waweze kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta hiyo ya fedha katika kuimarisha na kukuza biashara zao sambamba na kuwakaribisha wananchi kushiriki kwani hakuna kiingilio.
‘’Niseme kwamba Njia mbalimbali tutakazotumia katika kutoa elimu ya fedha kwa umma ni pamoja na machapisho(vipeperushi, na mabango madogo); uandishi wa insha; gari la matangazo; semina; maonesho ya bidhaa za fedha; majukwaa ya kidigitali(mfano; simu za kiganjani), mitandao ya kijamii, vyombo mbalimbali vya habari(TV, Radio, Magazeti) pamoja na burudani’’Alisisitiza Dkt.Mwamwaja
Maadhimisho hayo ya tatu ya wiki ya huduma za kifedha yaanaanza leo katika Viwanja vya Shekh Amri Abeid Jijini Arusha yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa siku ya jumatano tarehe 22/11/2023
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...