Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa benki hiyo leo wamekabidhi msaada wa fedha taslimu kiasi cha sh milioni 10, chakula, nguo na mablanketi kwa wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara.

Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20, pamoja na fedha taslimu unahusisha mchele, maharage, unga na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na  jumla ya tani 3.5.

Msaada huo umekabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki ya NBCM  Bw Godwin Semunyu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Bw Semunyu aliekuwa ameambatana na baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliowakilisha wafanyakazi wengine wa benki hiyo, alisema NBC inatoa salamu za pole kwa wahanga wa tukio hilo, serikali na Watanzania kwa ujumla na kwamba imepokea kwa huzuni kubwa taarifa za athari zilizotokana tukio hilo ikiwemo vifo na upotevu wa mali.

Alisema benki hiyo inaungana na watanzania kwa ujumla katika kuwafariji wahanga wa tukio hilo kwa hali na mali na zaidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wote  waliojeruhiwa na waliopoteza maisha katika janga hilo.

“Tumeamua kutumia kiasi tulichanacho kama taasisi na pia kama wafanyakazi mmoja mmoja kuwasaidia ndugu zetu wanaopitia wakati mgumu kwasasa kutokana na janga hili baya. Pamoja na fedha kiasi pia tumewaletea vyakula mbalimbali ikiwemo unga, mchele, maharage na mahitaji muhimu kama vile mablanketi na shuka ili viwasaidie kwa kipindi hiki cha mpito. "

“Pia tunashukuru sana serikali yetu na jamii kwa ujumla kwa kusimama imara na kuonyesha ushirikiano mkubwa katika kusaidia wahanga na majeruhi wa janga hili. Tumefarijika kuona wahanga wanaendekea kupata faraja kupitia misaada mbalimbali inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali pamoja na serikali. Nasi tunaahidi kuendelea kusaidia zaidi kadili iwekezanavyo,” alisema Semunyu.

Akipokea msaada huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz aliishukuru benki ya NBC na wafanyakazi wa benki hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa mafuriko hayo   hatua inayothibitisha nia ya dhati ya benki hiyo katika kushirikiana na jamii.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (wa tano kulia) akiwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kukabidhi kwa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (wa tatu kushoto) msaada wa fedha taslimu kiasi cha sh milioni 10, chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (aliebeba mafuta) akiwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kushusha shehena ya mahitaji  ikiwemo chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Anaeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (kushoto) Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Singida Bi Asia Chambega (wa pili kulia) akikabidhi kwa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (wa tatu kushoto) msaada wa chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.


Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Babati Bw Rodgers Masolwa (wan ne kulia) sambamba na Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki hiyo Bi Brendansia Kileo (wa tatu kulia) wakikabidhi kwa  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jimmy Yonaz (wa tatu kushoto) msaada wa chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.

Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC wakishusha shehena ya chakula, nguo na mablanketi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko Wilayani Hanang, mkoani Manyara. Msaada huo wenye jumla ya thamani ya sh milioni 20 umekabidhiwa leo wilayani humo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...