Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) imeibuka mshindi wa kwanza ya umahiri katika uaandaji wa taarifa za mahesabu kwa mwaka unaoishia 2022, kwa Sekata ya Fedha na Benki hapa nchini katika kundi la Taasisi za Fedha.

Utoaji wa tuzo ulioratibiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ulifanyika Disemba 01, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo washindi katika makundi mbalimbali walikabidhiwa tuzo zao na CPA. Jamal Kassim Ally, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Zanzibar na kwa upande wa KCBL, tuzo hiyo ilipokelewa na Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) Godfrey Ngura
 
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) Godfrey Ngura amesema wanamshukuru Mungu kwa tuzo hii na ni wazi kwamba watumishi wao wanafanya kazi kwa umahiri wa hali juu sana, hakika anawapongeza na nawaomba waendelee kufanyakazi kwa kuzingatia ubora na taratabu zote za ndani na za kimataifa.

"Kwetu ni Ushindi mkubwa na sana na ni ushindi wa Tasnia ya Ushirika nchini na tumetuma ujumbe kwamba ushirika unaweza lakini pia hakuna aliyeamini kwamba Taasisi yetu baada ya kupitia changamoto mbalimbali za kimtaji na Uendeshaji ndani ya miaka mitatu inakuwa benki bora inayoweza kuandaa hesabu zake vizuri na zikahakikiwa na vyombo husika nchini na kuibuka kidedea" Alisema  Ngura

Pia ametoa shukrani kwa Uongozi wa Bodi, wanahisa na Wateja wao kwa kuendelea kuwaamini pamoja na historia ambayo sio chanya sana na tulipoanza mageuzi haya Benki ilikuwa na Taarifa za Mashaka na zisizoridhisha  kwa takribani miaka 10 iliyopita lakini ndani ya miaka miwili tumeweza kutengeneza hesabu zilizopelekea kuwa kidedea.

Ngura amesisitiza kuwa Benki hiyo inakwenda kufanya mapinduzi kwa kuanzisha Benki ya Kitaifa ya Ushirika hivyobasi hiki ni kiashiria cha msingi  bora kitakachopelekea ubora, uimara unaozingatia Uhimala  na ubunifu katika kuandaa hesabu zake.
Washindi mbalimbali wa Tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2022 (Best Presented Financial Statements for the Year 2022 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) Godfrey Ngura akiwungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2022 (Best Presented Financial Statements for the Year 2022 Awards) zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...