Na.Khadija Seif Michuziblog

BODI ya Utalii nchini kwa kushirikiana na nyumba ya Vipaji vya sanaa (THT) wametambulisha rasmi programu ya kutembelea vivutio vya Utalii kipindi hiki cha Msimu wa Sikukuu.

Akizungumza na Wanahabari Leo Disemba 02,2023 Ofisi za Bodi ya Utalii nchini (TTB) MKurugenzi wa Bodi hiyo Damasi Mfugale amesema kwa kutambua mchango unaofanywa na nyumba hiyo ya Vipaji wameamua kushirikiana nao ili kutangaza na Kuhamasisha watalii kutembelea vivutio vya Utalii.

''Kipindi hiki cha Sikukuu za kristmas na Mwaka mpya tumeona ni nafasi nzuri kwa Watanzania kutembelea vivutio hivi ambapo pia watatakiwa kushiriki kujibu maswali mbalimbali katika mitandao yetu ya kijamii na watakaobahatika kushinda watapatiwa nafasi ya kutembelea vivutio hivyo kwa upande wa Kusini."

Hata hivyo Mfugale ameongeza kuwa vimeandaliwa vifurushi ambavyo watakaohitaji kutembelea vivutio hivyo wataweza kumudu gharama hizo.

"Vivufurushi hivyo ni Hifadhi ya Mikumi kwa shilingi 450,000,Arusha kwa shilingi 555,000 ,Ruaha 195,000,Mlima Kilimanjaro 1,900,000 pamoja na Mlima Meru 1,310,000.

Aidha Kampeni hiyo imepewa jina la "Likizo time" ambayo imeanza rasmi Leo Disemba 02,2023 na kutarajiwa kuisha mapema Januari 05,2023.

Pia ametoa wito kwa Watanzania kutembelea vivutio hivyo ambavyo vya kipekee na tunu ka nchi yetu.

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Damasi Mfugale akiwa na Mkurugenzi wa Nyumba ya Vipaji vya Sanaa (THT) Kemi Mutahaba mara baada ya Kuzindua Kampeni ya "Likizo time" inayolenga kuhamasisha watalii kutembelea vivutio kipindi hiki cha Sikukuu za kristmas na Mwaka mpya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...