Zaidi ya wanawake 100 wakiwemo wajane katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wanaratajiwa kupata mtaji kupitia kampeni ya Mama simama itakayowawezesha wanawake kuinua vipato vyao.

Mkurugenzi wa shirika la Chagua kurudisha tabasama (CKT) Dafroza Kyando amesema malengo yao ni kusimamaisha akina mama 100 na sasa wameanza na akina 10 wa mji wa Makambako ikiwepo kuwapa elimu wezeshi huku pia wakiwalenga wajane kutokana na mazingira yao.

"Malengo ni kusimamisha akina mama 100 na tumeanza akina mama 10 wajane kwa kuwapa elimu wezeshi na mitaji ambayo itatokana na kila mtu amepata wazo gani ili apewe huo mtaji"amesema Dafroza.

Aidha amesema sababu kubwa ya kuja na mpango huo hususani kwa wajane ni kutokana na hali walizo nazo baadhi ya wanawake ambapo wanahitaji kukuza uchumi wao pamoja ili kuimarisha familia ambapo wameanza na mji wa Makambako huku wakitarajia kufikia wanawake wengi mkoani Njombe.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...