Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ameutaka uongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na viongozi wengine wa taasisi za umma na binafsi kutoa kipaumbele kwa vijana waliofudhu mafunzo ya Jeshi la Akiba( Mgambo) kuimarisha ulinzi na shughuli nyingine za ujenzi wa Taifa.

Ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo kwa askari 106 wilayani humo akiwataka askari hao kuzingatia kiapo na kuwa mstari wa mbele kupambana na maovu.

"Niwahakikishie vijana wetu Serikali itaweka kipaumbele kuhakikisha inapotokea fursa yoyote mnapewa kipaumbele iwe shughuli zilizo Chini ya Halmashauri ikiwemo Ulizi, kusimamia makusanyo ya mapato...

" Kukimbiza mwenge na nafasi za JKT mnachopaswa kuzingatia ni uadilifu na kuviishi viapo mlivyo apa baada ya kuhitimu mafunzo,"amesema.

Amewataka pia wahitimu hao kuangalia uwezekano wa kuniendeleza kielimu kwa kusoma kozi mbalimbali ikiwemo Udereva, ufundi Umeme na Uwashi kujijengezea ujuzi na sifa za kuwa na vyeti ambavyo vitawasaidia kipindi zitakapo tokea nafasi za ajira serikini kupewa kipumbele kwa kuwa na sifa za ziada.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...