Na Mwandishi Maalumu – aliyekuwa wilayani Siha

27/12/2023 Wataalamu wa afya nchini wametakiwa kipindi wanachokuwa likizo kutenga muda wa kufanya utalii wa ndani ili kujionea vivutio mbambalimbali vilivyopo kwa kufanya hivyo kutasaidia kupumzisha akili zao.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utalii tiba unavyoendana na utalii wa vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

Mhe. Dkt. Mollel ambaye aliambatana na wataalamu wa Taasisisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutembelea shamba la wanyamapori Serval Wildlife lililopo wilayani Siha kwaajili ya kufanya utalii wa ndani.

Alisema wataalamu wa afya wanafanya kazi kubwa na ngumu ya kuokoa maisha ya wagonjwa hivyo basi ni muhimu kipindi wanapokuwa likizo wakatenga muda wa kupumzisha akili zao kwa kutembellea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini kwa kufanya hivyo wataweza kufanya kazi zao vizuri zaidi kwani ukiwa na akili iliyotulia utaweza kufanya kazi ngumu kirahisi.

“Leo nimekuja hapa kuwapa zawadi wataalamu wa JKCI waliyopewa na Mhe.Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, zawadi hii tumewapa baada ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha miundombinu ya afya alisema tuanze kufanya utalii tiba na taasisi ya kwanza kuelewa hili jambo na kuanza kulitekeleza ni JKCI na wengine wakafuata”,.

“Nimekuja hapa kuwaonesha jinsi utalii tiba unavyoendana na utalii wa kawaida wameona utalii uliopo kwa kujua kwao kutasaidia kuwajulisha wagonjwa kutoka nje ya nchi wanaowatibu kuwahamasisha kutembelea vivutio vilivyopo pindi watakapoona”, alisisitiza Mhe.Dkt. Mollel.

Kwa upande wake Fawad Hamoud Mkurugenzi Mtendaji wa shamba la wanyamapori Serval Wildlife aliwashukuru wataalamu wa JKCI kwa kutembelea shamba hilo na kusema kuwa JKCI imekuwa ni taasisi ya kwanza kutembelea mahali hapo na kupata nafasi ya kulisha wanyama na kupiga nao picha.

Fawad alisema katika shamba hilo wanajishughulisha na ufugaji wa wanyamapori wambao ni tofauti na ufugaji wa wanyama wengine walioko Zoo kwani ukiwa katika shamba hilo unakaa karibu na Wanyama akiwemo simba unawalisha chakula na kupiga nao picha.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutupa nafasi ya kufanya uwekezaji mahali hapa na tunatumia nafasi hii kutangaza utalii , tunapokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuona wanyama tunawaomba wananchi mje mahali hapa kulisha wanyama na kupiga nao picha”, alisema Fawad.

Nao wafanyakazi wa JKCI waliotembelea vivutio hivyo walimshukuru Waziri wa Afya kwa kuwapa nafasi hiyo na kusema kuwa wameona utalii uliopo na hiyo itawasaidia kutangaza vivutio hivyo kwa wagonjwa wanaowatibu pamoja na wataalamu wa afya wanaokuja kufanya kambi za upasuaji wa moyo kutoka nje ya nchi.

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walikuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa huduma za upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi na kutumia nafasi hiyo kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika wilaya hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...