Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Meja Jenerali  Paul Kisesa Simuli Ikulu Zanzibar aliyefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe: 28 Disemba 2023.

Rais Dkt.Mwinyi amesema  Zanzibar sekta kuu ya uchumi ni utalii ni fursa kwa Uganda kufanya biashara na uwekezaji  pamoja na fursa nyingine zilizomo katika uchumi wa buluu .

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amemtaka Balozi Simuli kudumisha ushirikiano na kubadilishana taarifa za ulinzi na usalama eneo la mpakani kati ya Tanzania na Uganda.

Naye Balozi Simuli amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya kuibadilisha Zanzibar kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...