Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu EWURA ambaye ni Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Mha. Exaudi F. Maro( aliyesimama) akisoma hotuba ya Ufunguzi wa kikao cha Maandalizi ya Kongamano la Wadau wa gesi asilia iliyoshindiliwa kitakachofanyika Januari 2024, jijini Dodoma, leo 21 Desemba 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo.

..................

Mkutano wa pamoja wa wadau wa gesi asilia ILIYOSHINDILIWA (CNG) nchini kwa ngazi ya Serikali unatarajiwa kufanyika Januari 10, 2024 kwa lengo la kuchagiza uwekezaji wa CNG ili kukidhi mahitaji ya nishati hiyo kwenye magari na shughuli nyingine za uzalishaji.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mha. Exaudi Fatael Maro, akifungua kikao cha maandalizi ya kongamano hilo, leo, tarehe 21 Desemba 2023 jijini Dodoma, amesema lengo la kukutanisha wadau, ni kujadili na kupata suluhu ya changamoto zinazoikabili sekta ndogo ya gesi asilia kwa upande wa CNG.

“ Ni matarajio yetu kuwa, kupitia kikao hiki, tutaweza kuandaa utaratibu wa utoaji elimu kwa wawekezaji na watanzania kwa ujumla kuhusu CNG.” Alisema.

Mha. Maro amewahisi washiriki wa kikao hicho kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi, Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira, Shirika la Taifa la Utafiti wa mafuta na gesi, Shirika la Viwango na EWURA kuimarisha ushikiano na kila taasisi husika kutekeleza wajibu wake ili kufanikisha kongamano hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya, ameeleza kuwa, kwa kuwa EWURA ndiye msimamizi wa miundombinu ya huduma ya CNG, itaendelea kutimiza wajibu wa kuhakikisha uwekezaji kwenye sekta hiyo, unafanywa kwa mujibu wa utaratibu ulioanishwa kwenye sheria na kanuni.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu EWURA ambaye ni Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Mha. Exaudi F. Maro( aliyesimama) akisoma hotuba ya Ufunguzi wa kikao cha Maandalizi ya Kongamano la Wadau wa gesi asilia iliyoshindiliwa kitakachofanyika Januari 2024, jijini Dodoma, leo 21 Desemba 2023. Kulia ni Mkurugenzi wa Gesi Asilia EWURA, Mha. Poline Msuya na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo.

Washiriki kutoka taasisi mbalimbali za Serikali wakiendelea na kikao cha maandalizi ya Kongamano la Gesi Asilia iliyoshindiliwa, linalotarajiwa kufanyika Januari 2024, kujadili mkakati wa kuimarisha uwekezaji kwenye eneo hilo, jijibi Dodoma, leo 21 Desemba, 2023,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...