Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuwaweka mazingira mazuri wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kufanya biashara zao katika maeneo yaliyobora na yakisasa kwa lengo la kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati alipokuwa akiweka jiwe la Msingi katika wa Mradi wa Soko la Chuini Kwanyanya Wilaya ya Magharibi “A” ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesema kuwa Serikali imeamua kuyajenga masoko hayo kwa kuwaondolea changamoto wafanya biashara wadogo wadogo hivyo ni lazima kuhakikisha masoko hayo yanawanufaisha wazanzibari na hayuko tayari kuwasaliti Wazanzibari kwa kuruhusu wakandarasi waliokosa sifa za kujenga Miradi Mikubwa ya kimaendeleo na kuitia hasara Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi kwa ujumla.


Mhe. Hemed amesema kwa kipindi kirefu wajasiriamali walikuwa wakilalamika juu ya kutokuwepo maeneo rasmi ya kufanyia biashara zao ambazo zinawasaidia kuwapatia kipato ambacho kinawaondolea umasikini hivyo Serikali itaendelea kuwawezesha kwa kuwapatia mitaji na mikopo nafuu ili kuweza kujimudu na kiuchumi.


Makamu wa pili wa Rais amesema ni vyema Viongozi kuwajibika na kutenda haki kwa kuwatumikia kwa moyo thabit wananchi wao ili kuunga Mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi ya kuwaletea Maendeleo Wazanzibari wote.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewapongeza Mkandarasi na Mshauri elekezi wa Ujenzi wa Mradi huo kwa hatua nzuri waliyofikia katika Ujenzi huo na kuwataka kuendelea kumalizia Ujenzi huo kwa kufuata makubaliano ili soko hilo likamilike kwa wakati na kiwango cha Ubora wa hali ya juu.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe Massoud Ali Moh'd Mohamed amesema Mhe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ni mwana Mapinduzi aliekamilika kwa matendo yake na uzalendo wake kwa Zanzibar sambamba na kuzidumisha fikra za waasisi wa Mapinduzi zilizoelekeza katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Amesema kuwa miongozo inayotolewa na viongozi wakuu wa nchi diko kulikopelekea leo hii kufikia kuwekewa jile la msingi soko hilo kwa maslahi ya waananchi pamoja na wafanya biashara hivyo Wizara itahakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati na kiwango kilichokusudiwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi Maalum vya SMZ Ndugu Issa Mahfoudh Haji amesema Mradi wa Ujenzi wa Soko la Chuini utajumuisha Soko pamoja na Stand kuu ya Daladala ili kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa eneo hilo na wananchi wanaofika kupata huduma eneo hilo.


Amesema kuwa kukamilika kwa soko hilo litawapunguzia wananchi wa chuini na vijiji jirani kero ya kufuata huduma masafa ya mbali, ambapo zaidi ya Bilioni 32 zitatumika hadi kukamilika kwa amradi wa Ujenzi wa Soko la Chuini Kwanyanya na kutoa nafasi kwa wafanyabiashara elfu mbili na mia tatu(2,300) kufanya biashara zako Sokoni hapo na linatarajiwa kutoa ajira kwa watu zaidi ya 5000 kwa wakati mmoja.

Mapema Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amemuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais kuwa Serikalini ya Mkoa itahakikisha inasimamia vyema soko hilo na masoko mengine ili kuhakikisha wafanya biashara wanadumisha usafi ili kulienzi kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Amesema kuwa kufanya hivyo ndio kuyaenzi Mapinduzi matukufu pamoja na kuezi zile fikra na mawazo ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume ambazo bado viongozi wakuu wanazienzi fikra hizo kwa vitendo.

Mshauri elekezi kutoka Wakala wa Mjengo (ZBA) Bibi Shadya Mohd Fauz amesema Mradi wa Ujenzi wa soko la chuini umefikia 75% ambapo kwa sasa upo katika hatu kumalizia ili liweze kukabidhiwa kwa Serikali.


Shadya amesema awali soko hilo liitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi December mwaka huu, lakini kutokana na chamgoto mbali ikiwemo kutopatikana kwa Local material na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha zimezorotesha ukamilikaji wa soko hilo hivyo ilinatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Machi 2024.
 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...