Na Ashrack Miraji Same kilimanjaro

MWENYEKITI  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha  Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Azza  Karisha amehitimisha mashindano ya Samia Cup yaliyokuwa yanachezwa kwenye Tarafa Gonja katika jimbo la Same Mashariki.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo Anne Kilango Malechele yenye lengo la kuhamasisha michezo sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihamasisha michezo kwa vitendo.

Katika mashindano hayo yamehitimishwa kwa mchezo wa fainali kuzikutanisha timu ya Ulimbo FC kutoka Kata ya Mtii  na Vuje FC kutoka kata  Vuje ambapo timu ya Ulimbo  FC iliibuka mshindi kwenye fainali hiyo na kutangazwa kuwa Mabingwa wapya.

Akizungumza wakati akihitimisha michuano hiyo ya Samia Cup,   Mwenyekiti huyo wa UVCCM amemshukuru Anne Kilango  kwa kuamua kuanzisha mashindano  ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Amesema mashindano hayo yamekuwa na tija kubwa kwa vijana kwa maana ya kujenga umoja, upendo, mshikamano  pamoja na kuimarisha afya zao.

"Niendelee kumshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa ambaye ndiye Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassani na serikali yake kwa namna ambavyo amewajali wananchi wa tarafa ya Gonja kwa kuwaletea fedha nyingi za maendeleo katika sekta mbalimbali, " amesema Karisha.

Pia amewaomba wananchi wa Gonja kuendelea kumuunga Mkono Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani na  Mbuge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango na CCM kwani ndicho  Chama pekee kinachoweza kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha  katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo ameongoza upandaji miti kwenye shule ya  Msingi Vuje mwendelezo wa utekelezaji wa kampeni ya Utunzaji wa Mazingira na kuifanya Same iwe ya kijani.

Kwa upande wake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki amesema jimbo hilo lina tarafa tatu tarafa ambapo mbili wamemaliza mashindano hayo bado tarafa moja kila tarafa inapaswa kutoa mshindi wa kwanza mpaka watatu.

Ameongeza baada ya hapo watapata timu  tisa ambazo zitaunda tena mashindo ya Samia Cup washindi wa tatu wanaopatikana kwa kila tarafa watapatiwa zawadi baada ya mashindano hayo kukamilika  na kumpata mshindi wa jimbo wa ligi ya Samia Cup.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...