Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), mwishoni mwa wiki alipamba msimu wa kwanza wa Tamasha la Bima Festival lililoratibiwa na benki ya Exim Tanzania huku akitoa wito kwa kampuni za bima na taasisi za fedha nchini kuongeza ufadhili wao kwenye sekta ya michezo ili kuchochea zaidi kasi ya ukuaji wa sekta hiyo inayokua kwa kasi.




Zaidi Bw Mwinjuma aliziomba taasisi hizo kubuni huduma mbalimbali zinazolenga kuwasaidia wadau wa sekta ya michezo na burudani nchini.

Katika tamasha hilo lililoratibiwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini zikiwemo kampuni za Alliance life Assurance Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Jubilee Allianz General Insurance Company Limited, Strategis Insurance Company Limited, The Heritage Insurance Tanzania na kampuni wateja wa benki hiyo ikiwemo kampuni ya bidhaa za plastic ya CELLO pamoja na kampuni ya uchimbaji madini ya Taifa Mining, ilishuhudiwa timu ya mpira wa miguu ya Exim ikiibuka mshindi wa jumla kwenye mashindano ya mpira wa miguu yaliyohusisha wadau wote.

Akizungumza wakati akizindua tamasha hilo Naibu Waziri Mwinjuma pamoja na kuwapongeza wadau hao kwa kuandaa tukio hilo lililotoa fursa ya kufurahia pamoja, kubadilishana mawazo na kujengeana ufahamu zaidi kuhusu huduma zao, aliwasihi wajitokeze zaidi kuunga mkono shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau wa michezo na burudani nchini kwa kudhamini shughuli zao mbalimbali na kuwatumia kwenye hamasa za kibiashara yakiwemo matangazo.

“Mchango wenu unaweza kutafsiriwa katika maeneo mengi ya kimichezo lakini msisitizo wangu nauweka zaidi katika udhamini wa matukio mbalimbali ya michezo husani katika uibuaji wa vipaji na kusaidia vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi mbalimbali hapa nchini ikiwemo ligi Kuu. Zaidi pia niwaombe muendelee kubuni huduma za bima na huduma za kifedha mahususi kwa wanamichezo na wasanii ili muwasaidie kulinda afya na kazi zao na zaidi kuwajenga kiuchumi.’’ Alisema.

Zaidi Bw Mwinjuma aliipongeza benki hiyo kwa jitihada zake za kukuza michezo hapa nchini kupitia msaada wa vifaa vya michezo inavyotoa kwa shule za msingi na sekondari katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

‘Mmeonyesha dhamira na nia njema ya kuinua vipaji vya vijana na kuwezesha maendeleo ya michezo nchini. Tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuendeleza michezo na tunawashukuru kwa kuwa wabia wetu katika kufanikisha malengo yetu ya kitaifa katika sekta hii.’ Alisema huku pia akionesha matumaini makubwa kuwa tamasha la Exim Bima Festival litakuwa na mafanikio makubwa na litaleta matunda yaliyotarajiwa.



Awali, akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki hiyo Bw Sumit Shekhar, alisema kupitia tamasha hilo litakalokuwa likifanyika kila mwaka, benki hiyo imejipanga kutumia vema fursa ya michezo na burudani kuboresha mahusiano yake na wadau wake mbalimbali wakiwemo wateja, wadau wa bima, wafanyakazi, mamlaka mbalimbali zinazosimamia sekta ya bima na benki pamoja na serikali.

“Tukiwa kama wadau muhimu wa sekta ya fedha na bima nchini kupitia huduma yetu ya Bima ijulikanayo kama ‘Bima tu Malipo Tuachie’ tumejipanga kuhakikisha tunalitumia vema tamasha hili kama mkakati muhimu wa kuboresha mahusiano baina yetu na wadau wetu tukiamini mahusiano ndio nguzo ya kwanza kwenye biashara yoyote na tamasha la Exim Bima Festival linakuja kama namna bora ya kutusaidia kufanikisha hilo,’’ alisema Bw Shekhar.

Akizungumzia ushindi wa jumla katika mashindano ya mpira wa miguu baina ya wadau hao, mfungaji bora katika mashindano hayo Bw. Calvin Kilua kutoka timu ya benki ya Exim alisema siri ya mafanikio ni timu yake kujiandaa vema kwa ajili mashindano hayo sambamba na kutafsiri vema maelekezo ya kocha wa timu hiyo ambae ni Meneja Rasilimali Watu Bw Mikidadi Ngoma.

“Baada ya mafanikio haya tunaamini kwamba tamasha lijalo litahusisha timu nyingi zaidi na ushindani utaongezeka. Hivyo tutaendelea kujiweka sawa kwa mazoezi zaidi kwa kuwa mazoezi pia ni afya na ukizungumzia afya ni moja ya agenda ya msingi kwenye huduma zetu za bima,’’ alisema Bw Stanley Kafu, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim.




Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa msimu wa kwanza wa Tamasha la Exim Bima Festival la benki ya Exim Tanzania lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo liliandliwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini zikiwemo kampuni mbalimbali za bima nchini. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki ya Exim Tanzania Bw Sumit Shekhar (Kulia).



Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki ya Exim Tanzania Bw Sumit Shekhar (aliesimama) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta bima nchini walioshiriki kwenye Tamasha la Exim Bima Festival lililoratibiwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini zikiwemo lilihusisha wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini. Wanaomsikiliza ni pamoja na Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) (kushoto)







Naibu Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) (Kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta bima nchini walioshiriki kwenye Tamasha la Exim Bima Festival lililoratibiwa na benki ya Exim Tanzania mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Tamasha lilihusisha wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki ya Exim Tanzania Bw Sumit Shekhar (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim Bi. Zainab Nungu (katikati), Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Bw Stanley Kafu (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Mali za benki ya Exim Bi Queen Siraki (Kulia)
Mwisho wa tamasha hilo, washiriki walipata fursa ya kushuhudia moja kwa moja kupitia screen kubwa mechi ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika baina ya Yanga na Al – Ahly


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Bw Stanley Kafu (wa tatu kushoto) akikabidhi vyeti vya utambuzi wa ushiriki na shukrani kwa baadhi ya wawakilishi wa kampuni za bima zilizoshiriki kwenye tamasha hilo.

Udambwi udambwi mwingi!


Hakika Exim Bima Festival ilikuwa ni furaha tu.


Baadhi ya vikosi vya timu washiriki wa mashindano ya mpira wa miguu kwenye tamasha hilo vinavyoundwa na wafanyakazi wa kampuni mbalimbali za bima nchini zikiwemo kampuni za Alliance life Assurance Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Jubilee Allianz General Insurance Company Limited, Strategis Insurance Company Limited, The Heritage Insurance Tanzania na kampuni wateja wa benki hiyo ikiwemo kampuni ya bidhaa za plastic ya CELLO pamoja na kampuni ya uchimbaji madini ya Taifa Mining.


Timu ya ushindi! Kikosi cha timu ya Benki ya Exim kilichoibuka mshindi wa jumla kwenye mashindano ya mpira wa miguu yaliyohusisha wadau wote.

Wadau wa tamasha la Exim Bima Festival kutoka Benki ya Exim na kampuni mbalimbali za bima nchini zikiwemo kampuni za Alliance life Assurance Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Jubilee Allianz General Insurance Company Limited, Strategis Insurance Company Limited, The Heritage Insurance Tanzania Limited na kampuni za wateja wa benki hiyo ikiwemo kampuni ya bidhaa za plastic ya CELLO pamoja na kampuni ya uchimbaji madini ya Taifa Mining, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa tamasha hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...